KERO Mbezi ya Mikojo! Imejaa Muda Wote, Si Ustaarabu Hata Kidogo Watu Kukojoa Hovyo! Ni Aibu Kubwa Sana

KERO Mbezi ya Mikojo! Imejaa Muda Wote, Si Ustaarabu Hata Kidogo Watu Kukojoa Hovyo! Ni Aibu Kubwa Sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Hali ya usafi katika maeneo mbalimbali ya Mbezi Mwisho, jijini Dar es Salaam, imekuwa ikilalamikiwa kutokana na watu kukojoa hovyo katika maeneo ya wazi, hali inayosababisha harufu kali ya mkojo na kuacha mazingira kuwa machafu.

Kuanzia Mbezi Mwisho hadi Stendi ya Magufuli, baadhi ya maeneo yameonekana kuwa na harufu ya mkojo, huku watu wakikojoa hovyo kutokana na ukosefu wa vyoo vya kutosha.

Ukienda katika maeneo yenye vibanda vya wafanyabiashara, utakutana na chupa za mikojo zilizotupwa hovyo, huku hali ikiwa mbaya zaidi katika maeneo ya stendi ambako baadhi ya watu hufanya haja ndogo katika maeneo ya wazi.

Hali hiyo imekuwa ikisababisha michirizi ya mkojo kuonekana katika maeneo mbalimbali, jambo ambalo linaathiri usafi na taswira ya eneo hilo.

Kiuhalisia, hali ni mbaya na inaweza kuwa hatari kwa afya ya jamii endapo kutatokea mlipuko wa ugonjwa, kwani mazingira machafu yanaweza kuongeza hatari ya kuenea kwa magonjwa.

Kwa sababu hiyo, Manispaa ya Ubungo inatakiwa kuongeza vyoo katika Stendi ya daladala za magari yanayoenda Mlandizi na Tegeta. Kwa sasa, eneo hilo lina choo kimoja pekee, licha ya kuwepo kwa idadi kubwa ya wafanyabiashara, abiria na wapiga debe wanaohitaji huduma hiyo.

Aidha, stendi ya magari yanayoenda Kinyerezi nayo haina choo, hali inayochangia baadhi ya watu kujisaidia katika maeneo ya wazi.
 
Kuna mtu mtu sasa hv yupo kariakoo, ameenda ktk mishe mishe, muhindi kazingua Ana buku tu mfukoni, ni nauli yakumfikisha nyumban majumba 6,kabanw na mkojo unadhan atafanya nini zaid ya ku tafuta chocho ajibanze alimwage, 😂
 
Uko sahihi,ila pale choo cha stendi cha wanaume ndio balaa,kuna siku nilikuta maji na mikojo imezagaa mle ndani nikasema aisee,kweli kuishi Dar ni kazi sana...
 
Back
Top Bottom