Mbinguni sio salama, ni propaganda tu!

Story ya Adam na Hawa ni ngumu.
Ilikuwa hivi,,katika nchi ya sumeria watu walianza kuwa civilized na kuanza kuishi pamoja,baadae kidogo kukatokea mtawala akiitwa hammurabi akaandika sheria za kuguide raia wake,kipindi hicho ,jamii zikaanza kuunda tawala,kukawepo akaddian kingdom,ikazaa mesopotamia na kisha ikazaa Asyrian,hawa asyrian ulikuja kuwa utawala wa nguvu baada ya kuupindua utawala wa babelyon.

So miongoni mwa watawala wa mwanzo wa Asyrian,alikuwepo ADAM,
Fastforward,waandishi wa kiyahudi sasa kwa kusikia habari za Adam mfalme wa asyrian,,katika fasihi zao ndo wakaja na habari miaka mingi mbele kuwa Adam ndo kiumbe cha mwanzo kuumbwa.
 
kwahiyo alipelekwa eden kulima,duh nisivyopenda kazi ya kulima mi ningekimbia tu
 
Nilikuwa najiuliza huyu jamaa mbona anaandika vitu vya hovyo na mwandiko wa ajabu, anatumia nguvu nyingi kwenye hoja zake.
Kumbe una ugomvi na Mungu!
Eti Eden siyo duniani
Unaandika mavitu haya uhalisia
 
sasa kila mtu akianza ya hizo story tutapakimbia humu
 
The point is that, Meko fool lacks the mental capacity to serve this country as a local government chairman, sorry I mean a president.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmh! Haya Mambo ni pasua kichwa kweli kweli, haya ngoja watu wameng'enye halafu waje.
 
Hapa panafurahisha na kufikirisha kidogo.
 
Mungu ni Mungu sababu yeye n Mungu hua hajielez na huwezi muelewa "God is not fair He's just" na hutakuja kumuelewa mpaka apende yeye umeuelewe we umeona umeandika kitu Cha point but n ujinga tu na ndo maana akasema nimeifanya hekima ya mwanadam kua n upumbavu.

Na Yesu aliwajibu wanafunzi wa yohane mbatzaji ana heli asiekwazika nami kuna muda Mungu atakukwaza na anajua ilo ila anasema ana heri asiekwazika nami by the way tunaitazamia Mbingu mpya ufalme mpya.

Kwa ujasili na kwa iman tunausubilia ufalme wa Mungu under the King himself Jesus Christ.

Ni heri uamini uonekane mjinga kuliko kujifanya mwelevu afu ukapotea.

Believe in Christ and He shall show u his ways God is really and He's love akuokoe kwa mapenzi yake
 
Nashukuru kwa uelewa wako Ila imeelezea Sana kutokana na historia ya biblia....

Kwenye Uislam. Ulivyoelezea kuumbwa Adam

Eden Garden

#NABII ADAM.
Allah, Kitu cha kwanza kukiumba ulimwenguni ni Qalam ambayo ameiumba kwa ajili ya kuandika mema na maovu ya viumbe.
.
Aliumba Lauhul-Mahfuudhna vyenginevyo.
.
Allah aliumba mbingu saba (7) Kwa Siku Sita (6) katika matabaka mbalimbali pamoja na mchanga (ardhi) siku ya Jumaamosi.
.
Aliumba majabali katika siku ya Jumaapili.
.
Miti siku ya Jumaatatu.
.
Vitu vyote vyenye kuchukiza aliviumba Allah katika siku ya Jumaanne.
.
Nuru siku ya Jumaatano.
.
Viumbe katika siku ya Alhamis.
.
Na mwisho alimuumba Adam katika siku ya Ijumaa nyakati za Alaasiri ndio siku ya mwisho ambayo wanaadamu wote wataondoka ulimwenguni.
.
Lakini kabla ya kuumbwa Nabii Adam, Allah alikuwa tayari amekwishawaumba majini ambao walifanya ufisadi katika ardhi na walimwaga damu za wengine.
.
Hatimae Allah aliwapelekea majini hao jeshi la malaika na wakateketezwa majini wote.
.
Mara tu baada ya Allah kuwateketeza majini hao, Malaika Jibriil alimbakisha mmoja katika kizazi cha majini aliyeitwa AZAAZIIL (Iblis) kwa vile jinni huyo alimuabudu sana Allah, hivyo Allah alimuweka pamoja na malaika peponi.
.
Iblis aliendelea kumwabudu Allah mpaka akafikia kuitwa Abaasijda, kutokana na wingi wa sijda zake kumsujudia Allah.
.
Hivyo ijapokuwa hakuumbwa kwa nuru (aliumbwa kwa moto), lakini Iblis alishirikiana na malaika katika ibada kumwabudia Allah.
.
Siku moja Allah aliwadokeza malaika kuwa anataka kuumba kiumbe mwengine duniani.
.
Malaika wakafikiri mambo yaliyowatokea kabla ya Adam, na jinsi wale majini walivyofanya ufisadi katika ardhi.
.
Hivyo malaika hao wakasema kwa kumuuliza katika quran tukufu;
“Ewe mola unataka kuweka katika ardhi anaetaka kufanya ufisadi na kumwaga damu, kama walivyomwaga damu waliopita.
Au unataka kuleta kiumbe atakaekuabudu kwa wingi?
Na je! Sisi tumepunguza kitu katika ibada yako? Na hali sisi tunakutukuza na tunakusabbihi kila usiku na mchana?”.
.
Nae Allah akawaambia katika qurani tukufu;
“Mimi ninajuwa vile msivyovijuwa nyinyi”.
.
Kutokana na uchamungu wao malaika wakasema;
”Basi aumbe Allah vile anavyovipenda katika viumbe.
Lakini hawatokua viumbe hao wabora na wajuzi kuliko Sisi"....

Hivyo Allah akauchukuwa mchanga inasemekana wa ufinyanzi na akaufinyanga kwa hatua mbalimbali mpaka ukafikia kwenye kiumbe mfano wa sanamu.
.
Hivyo Allah akasimamisha sanamu hiyo ya Adam kwa muda wa siku arubaini (40).
.
Na wakati ikiwa imesimama kila siku malaika walikuwa wakipita na kuiangalia sanamu hiyo iliyoweka uwanjani hapo.
.
Hivyo hapo sasa ikawa ni mwanzo wa fitna na kejeli kwa iblis kwani alihisi kiumbe huyo atakuja kupewa thamani kubwa kuliko wao, lakini mmoja wa malaika alipewa elimu ya kujuwa kitu cha baadae na Allah hivyo akawa anawatoa wasiwasi wenzake juu ya kiumbe hicho.
.
Katika siku ya arubaini Allah akaileta roho na kuanza kukipulizia kiwiliwili hicho.
.
Hapo Adam akapiga chafya na ndipo malaika wakamwambia Adam;
“EweAdam sema Alhamdulillah kwani Roho ndio kwanza imewasili”.
.
Adam hapo hapo kwa kushukuru akasema Alhamdulillah na Allah akamuitikia na ndipo Roho ikaingia machoni ambapo Adam akaona matunda ya aina kwa aina peponi.
.
Akaanza kuyatamani matunda yale ilhali roho haijafika hata tumboni, akataka pia kutembea wakati roho haijafika hata miguuni, na ndio maana mwanaadamu akawa ana tabia ya kuwa na pupa katika mambo yake siku zote.
.
Roho taratibu ikaingia kiungo kimoja baadaya chengine mpaka ikamalizia miguuni.
.
Hapo ndipo Allah akamuamrisha Adam apite mbele ya malaika na awatolee salam na hapo ikawa ni mwanzo wa salam katika Uislam.
.
Allah akasema, “Haya yatakuwa ni maamkizi kwa umma wako”.
.
Allah alimfundisha Adam majina ya vitu vyote duniani, pamoja na matumizi ya vitu hivyo.
.
Allah alivileta vitu hivyo mbele ya malaika na akawaambia;
”Nielezeni majina ya vitu hivyo ikiwa nyinyi ni wakweli”.
.
Malaika wakashindwa na wakajibu kumwambia Allah;
”Utakasifu ni wako Ewe mola, na sisi hatuvijui vitu hivyo ispokuwa vile ulivyotufundisha tu”.
.
Allah akamleta Adam na akamwambia avitaje vitu hivyo vyote, nae Adam hakusita akavitaja vitu hivyo vyote.
.
Hapo ndipo Allah akawaambia malaika;
“Ninayajuwa yale msiyoyajuwa, basi msujudieni Adam”.
.
Hapo malaika wote walisujudu ispokuwa Iblisi pekee akakataa na akafanya kiburi na akawa ni miongoni mwa waliokufuru..
 
Mungu aliumba mke na mume. Mke akazinguaga, then akamuumba Hawa.

Kuna jamaa mmoja alishalifafanua hili humu jf kuhusu Lilith. Tafuta utaelewa.

Alafu, watu wa kale wanaeza kaa muda mrefu pasipo kufanya mapenzi, broo.
 
Hizi sasa bange[emoji23][emoji23]
 
Dini na sayansi vinaendana. Dini inaelezea simple jambo ambalo kisayansi lina evolution kubwa mno.

Mf. Siku moja ya kwenye biblia (hasa za agano la kale ni kubwa na ndefu mno kuliko ya kisayansi au kisasa.)

The same, siku moja ya mbinguni ni sawa na miaka zaidi ya elfu ya duniani.

Upo uwezekano uumbaji wa Mungu kwa siku saba za kwenye kitabu cha dini, ni sawa na miaka mingi mno ambayo haielezeki kwenye Dunia yetu kisayansi

So, huenda ikawa kweli, kuna viumbe viliishi kabla ya mwanadamu, maana hata kisayansi, Dinosaurs na viumbe reptiles wa zamani walitokomeaga kwenye vilindi vya maji, kabla ya evolution of man.
 
Mwanzo 4: 16
Ndipo Kaini akaenda zake kutoka usoni pa Yehova na kukaa katika nchi ya Ukimbizi upande wa mashariki wa Edeni.

(hii ni baada ya Adam kutimuliwa eden)
Upo sawa pia, maanaa bustani ya edeni ilikuwa inaelea angani, na uliwekwa upanga kotekote ili binadamu asiweze kuingia.

Inaonekana ni kama vile mji wa kufikirika, au mji wa kwenye ulimwengu usioonekana
 
Kwa walio na free mind wataelewa huyu jamaa aliandika nini,ila wale wenzangu brain washed na hadith pamoja na mapokeo ya kiyahudi na kigiriki hawatamuelewa labda bahari ikauke,
Wafia dini nasemaje


Povu ruksaaaaa!
 
Kwaiyo Allah akujua apo kwamba ibilis atagoma kumsujudia Adam akatak kumchora
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…