Mbinguni sio salama, ni propaganda tu!

Mbinguni sio salama, ni propaganda tu!

ACHA KUPOTOSHA WATU WEWE UNAONEKANA HATA UNACHO ONGEA HUNA HAKIKA NACHO JE WAJUA EDENI IKO WAPI TUANZIE HAPO BAADA YA VITA KUU KUTOKEA MBINGUNI NDIPO SHETANI NA MALAIKA WAKE WALITUPWA DUNIANI AMBAPO MWANADAMU WA KWANZA ALIUMBWA HUMO NA PIA EVA AKAFUATA WOTE WAKIWA KATIKA BUSTANI YA EDENI NA SHETANI AKAMJIA EVA KWA UMBILE LA NYOKA HAPA TUNAONA SHETANI ALITUPWA DUNIANI NA AKAMTOKEA EVA KWA UMBILE LA NYOKA HIVYO INAMAANISHA BUSTANI YA EDEN ILIKUWAPO DUNIANI NA MUNGU YUPO KILA MAHARI NA UWEZA WAKE UPO KILA MAHALI ILA KAANDAA MAKAZI YA WATOTO WAKE AMBAO WALIIFUATA SHERIA YAKE NA MUNGU YUPO MBINGUNI KWENYE KITI CHAKE CHA ENZI
 
ACHA KUPOTOSHA WATU WEWE UNAONEKANA HATA UNACHO ONGEA HUNA HAKIKA NACHO JE WAJUA EDENI IKO WAPI TUANZIE HAPO BAADA YA VITA KUU KUTOKEA MBINGUNI NDIPO SHETANI NA MALAIKA WAKE WALITUPWA DUNIANI AMBAPO MWANADAMU WA KWANZA ALIUMBWA HUMO NA PIA EVA AKAFUATA WOTE WAKIWA KATIKA BUSTANI YA EDENI NA SHETANI AKAMJIA EVA KWA UMBILE LA NYOKA HAPA TUNAONA SHETANI ALITUPWA DUNIANI NA AKAMTOKEA EVA KWA UMBILE LA NYOKA HIVYO INAMAANISHA BUSTANI YA EDEN ILIKUWAPO DUNIANI NA MUNGU YUPO KILA MAHARI NA UWEZA WAKE UPO KILA MAHALI ILA KAANDAA MAKAZI YA WATOTO WAKE AMBAO WALIIFUATA SHERIA YAKE NA MUNGU YUPO MBINGUNI KWENYE KITI CHAKE CHA ENZI

Huyo aliyepo mbinguni ni Yehova Mkuu, na aliyepo akhera sijui peponi ni Allah HAO ni miungu tuu.

Mungu Mkuu Hana Anuani, anaishi pote katika yote.

Kusema MUNGU anakiti cha Enzi ni kukufuru, na matusi ya wazi Kabisa.
 
Huyo aliyepo mbinguni ni Yehova Mkuu, na aliyepo akhera sijui peponi ni Allah HAO ni miungu tuu.

Mungu Mkuu Hana Anuani, anaishi pote katika yote.

Kusema MUNGU anakiti cha Enzi ni kukufuru, na matusi ya wazi Kabisa.
Basi sawa ni mtizamo wako
 
viumbe wote hao walikuwa madume na majike.

Iweje kwa binadamu kuwe na mkwamo na kusua sua kwa uumbaji kiasi hicho?
Mwanamke wa kwanza aliye kuwa na Adamu alikuwa Lilithi!! lkn alikuwa na kipondo si cha kawaida! alikuwa anamtia vitasa Adamu, Mbishi, mnoko! kwa tabia hizi alimuasi Adamu!

Adamu akalalamika akarudi kwa Mungu kuomba tena ndo akapewa Hawa/eva mlaini! laini!...mpaka leo ndo hawa hawa!
 
Huyo aliyepo mbinguni ni Yehova Mkuu, na aliyepo akhera sijui peponi ni Allah HAO ni miungu tuu.

Mungu Mkuu Hana Anuani, anaishi pote katika yote.

Kusema MUNGU anakiti cha Enzi ni kukufuru, na matusi ya wazi Kabisa.
Heri,

Mosi, Aliyeumba yaani Mungu Baba rejea 1korintho 15:24-28 ambaye ndiye CHANZO HALISI aliumba Mbingu na nchi na sio Dunia na ulimwengu rejea mwanzo 1:1, Dunia na ulimwengu ni mfumo wa maisha unaoendesha maisha ya watu Kila siku uliotokana na miungu mbalimbali lakini halikuwa kusudi la muumba.

Pili, aliyetuumba hakuwa mbinguni Bali mahali pake na hakuna aliyekuwa anapajua ukirejea Mika 1:2-3 "Sikilizeni, enyi watu wa kabila zote; sikiliza, Ee dunia, na vyote vilivyomo; Bwana MUNGU na ashuhudie juu yenu, yeye Bwana kutoka hekalu lake takatifu. 3 Kwa maana, angalieni, Bwana anakuja akitoka MAHALI PAKE, naye atashuka, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka."

tatu, Mbinguni kulikuwa na kitu kingine tofauti rejea yeremia 44:17-18 "Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya. 18 Lakini tulipoacha kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, tumepungukiwa na vitu vyote; na kuangamizwa kwa upanga, na kwa njaa."

Pia huyo malkia wa mbinguni utamkuta katika ufunuo 12:1 "Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili." Huyo malkia wa mbinguni ndie alikuwa anatawala hata shetani au ibilisi haoni ndani kwa huyo ndie aliyekuwa ameteka uumbaji.huo mwezi chini ya miguu yake na taji ya nyota kumi na mbili ni mada ndefu inayohitaji Uzi wake.

Hitimisho
Aliyetuumba alimuumba Adam na Hawa ndani ya bustani ya Edeni na alimpa mtu mamlaka kubwa kuliko viumbe vyote kabla ya Ibilisi kuja kumdanganya Adam na Hawa rejea Zaburi 8:4-6 "Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? 5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; 6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake."
 
USALAMA WA MBINGUNI BADO NI MDOGO

Na, Robert Heriel

Wakati Mungu anaumba Mradi wake wa Dunia aliumba kila kitu kikiwa chema kabisa. Hakuna ambacho kilikuwa na kasoro, kila kitu kilikuwa kimekamilika. Hivyo yeyote unayemuona hapa duniani ujue amekamilika yaani yuko full completely. Hii Propaganda ya kusema mwanadamu hajakamilika ni hila, njama, ulaghai wa viumbe wasio na asili ya binadamu.

Kabla sijaenda mbali, nieleze kwa kifupi namna Mradi huu wa Dunia ilivyoumbwa na Mungu. Mungu aliiumba dunia kwa mfumo wa kutegemeana (Ecosytem) yaani viumbe vinategemeana. Kutegemeana huku ndio kunakamilisha mradi mzima wa dunia. Katika Mradi huu kuna aina nyingi za viumbe kulingana na asili yao walivyoumbwa. Mathaalani; Wapo viumbe walioumbwa kwa Hewa, wapo walioumbwa kwa maji, wapo walioumbwa kwa moto, wapo walioumbwa kwa Mwanga/ nuru wapo walioumbwa kwa udongo, wapo walioumbwa kwa mchanganyiko wa mada zaidi ya moja yaani labada maji na udongo, au hewa na mwanga.

Hivyo naweza kusema viumbe wapo aina zifuatazo kulingana na malighafi zilizotumiwa kuwaumba:

1. Viumbe wa umaji
2. Viumbe wa Umoto
3. Viumbe wa Uhewa
4. Viumbe wa Udongo/umadini
5. Viumbe wa Unuru/umwanga
6. Viumbe waliochanganya malighafi kama mwanadamu ambaye amechanganya umaji (ikiwemo damu), udongo na uhewa (Roho) chochote kikipungua katika mchanganyiko huo basi maisha ya mwanadamu aypo mashakani.

Kila kiumbe kimepewa Miliki au ufalme wake na watakaokitumikia. Mwanadamu amepewa dunia, na vyote vilivyopo duniani ni mali yake na vinamtumiikia.

Nikirejea kwenye Mada.

Adamu aliumbwa Duniani ambapo kiasili ndio kwake. Baadaye Mungu Akamchukua huyo Mtu akampeleka (Edeni) ambapo kiasili sio Duniani. Kumbuka Adamu akitolewa Duniani kupelekwa Edeni alikuwa pekeake kwa mujibu wa maandiko.

Baadaye Mungu akamuumba Hawa/Eva kupitia ubavu wa Adamu. Hii ni kumaanisha Eva/Hawa aliumbiwa Edeni. Najaribu kufikiri na kugundua kuwa Eva ni matokeo ya mchangiko wa malighafi za dunia na Edeni. Kupitia Ubavu wa Adamu, Eva alijipatia malighafi za dunia(udongo) na kupitia malighafi zingine zilitoka pale pale Edeni. Nadhani mpaka sasa unaweza anza kupata picha ya kuelewa tofauti baina ya mwanaume na mwanamke kiasili.

Lakini lazima tujiulize, wakati Mungu akiumba mradi wake mara zote alikuwa akikiri kuwa kila alichokifanya ni chema na hakika ilikuwa chema, lakini baada ya kumhamisha Adamu na kumpeleka Bustani ya Edeni ni kwa nini mawazo yake yalibadilika na kusema "Si vyema" "huyu mtu awe pekeake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye" na hapo ndipo akamuumba Hawa/Eva kupitia ubavu wake. Hii ni kumaanisha Kwa duniani Adamu ilikuwa vyema kuwa pekeake wakati Edeni haikuwa Vyema.

Lakini hapa panaweza kuleta hitilafu kwenye kufikiri, je ni Mungu huyo huyo aliyesema kila kitu ni chema na sasa amebalisha mawazo? Mbona Mungu sio kigeugeu?

Akili yangu inaenda nisikokujua inafikiri hivi, huenda Aliyemuumba Adamu siye aliyemuumba Hawa. Kwanini ninafikiri hivi? Pengine niseme sijui. Embu tuone.

Nafikiri Hawa aliumbwa kwa njama, hila, za Kumuangusha Adamu. Kumbuka Adamu kwake ni duniani, wala sio Edeni. Edeni ilikuwa inamwenyewe, je ni nani huyo?

Embu ona, Adamu analetwa tuu Edeni hapo hapo anapewa sheria ya kutokula Tunda la Mti wa Kati wa ujuzi wa mema na mabaya. Fikiria hapo! Punde anaumbwa Hawa/Eva kisha aliyeumbwa muda huo huo anakuwa wakwanza kula tunda. Bado hujashtuka. Akili yako inakuambia nini kuhusu aliyemwambia Adamu asile matunda ya mti wa kati wa ujuzi wa Mema na Mabaya kwani atakufa? Kisha aliyeumbwa Edeni anakula hilo tunda na anaenda kwa adamu akiwa hajafa, huoni adamu angeona aliyesema ukila utakufa angekuwa muongo? Kumbuka Mlengwa wa lile tunda kula hakuwa Hawa/Eva bali alikuwa adamu. Kama Adamu asingekula lile tunda ni wazi Eva asingepata madhara. Lakini hila za aliyemuumba Eva, na ndiye huyo huyo aliyemwambia ale ili ampe adamu amuaminishe kuwa hatakufa ili ale ndio zilimuingiza Adamu Mkenge, kula tunda la sumu, lenye kuua taratibu kizazi cha Adamu mpaka hivi leo. Bado hujaona kifo ni mradi wa viumbe fulani?

Baadaye tunapata habari za Nyoka akimdanganya Hawa/Eva ili akampe lile tunda Adamu. Lile Tunda lisingekuwa na madhara yoyote kwa Eva/Hawa kama Adamu asingelila. Mtihani ule ulikuwa unamhusu Eva/ Hawa. Hata hivyo Hawa/Eva hakudanganywa bali alifanya makusudi kwani tayari alikuwa anapewa oda na aliyemuumba(huyo aliyemwambia ampe mumewe lile tunda)

Nyoka(ambaye sio huyu atambaaye) ndiye alikuwa mmiliki wa ile Edeni. Kama Adamu alivyoambiwa atawale dunia.

Ili ujue Hawa/Eva alifanya kusudi kumuangamizA Adamu, angalia alivyoenda kumpa lile tunda Adamu ili alile, wala hakumpa maelezo yoyote kuhusu huko alikotoka zaidi ya kumwambia nimelila na lafaa kwa kula. Hakumwambia amekutana na nani. Habari hizo Adamu anakuja kuzifahamu baada ya Mungu kuja ambapo Eva/Hawa anasema kuwa amedanganywa na Nyoka, (Namuona Adamu akijiona mjinga akitumbua macho yake kama mtu asiyeamini kuwa kaangushwa bila kujua) Mungu akamwambia umeisikiliza sauti ya mke wako. Kumaanisha hakupaswa kumsikiliza bali yeye ndio asikilizwe.

Baadaye Adamu na Hawa wanatimuliwa Edeni, na kurudishwa Duniani tayari akiwa amekula tunda lenye sumu iuayo pole pole. Na Mmiliki wa Edeni anabaki kuwa mshindi.

Kilichokusudiwa kifanyike Edeni kimekamilika, Adamu hahitajiki tena Edeni hivyo kufukuzwa ndio suluhu.

Alifukuzwa, na hapo ndipo rasmi mwanadamu akaanza kukengeushwa na viumbe wa Mbinguni kwa kutumia mawakala zao waliopo huku duniani. Mara Mbinguni, mara peponi mara sijui Akhera.

Ati tutaishi na Mungu. Sirius! Kabla ya kuanguka hatukuishi na Mungu, hata sasa hatuishi na Mungu, na kamwe hatuishi na Mungu. Hata hao viumbe wengine hawajawahi kuishi na Mungu. Bali ni propaganda zao za kurubuni kizazi cha mwanadamu kzidi kuwa watumwa.

Nataka kusema nini?

Dunia haijawahi kuwa mbaya, ubaya unatokea nje. Bila Edeni pasingekuwa na mabaya yote yanayoendelea duniani. Edeni ndio kulikuwa na tatizo wala sio dunani.

Mbinguni wanaishi malaika, Mungu haishi Mbinguni wala haishi duniani.Mungu hana Anuani, popote yupo kwa wakati wote. Mungu hana Kiti cha Enzi. Mungu hana Ulinzi. Malaika ni viumbe walioumbwa kwa Mwanga mkali, wenye mfano wa mwanadamu lakini hawana miili kama yetu. Malaika wapo wa aina nyingi kulingana na kazi, maumbile, na Sifa. Wapo malaika wenye mbawa kuanzia mbili, tatu, nne, sita, kumi na mbili na kuendelea.

Huko Mbinguni ndipo matatizo yalipoanzia, Falme za Malaika zimegawanyika. Kuihubiri mbinguni ni kuidhalilisha dunia. Kuwatukuza Malaika ni kuwatukana wanadamu.

Ipo tabia baadhi ya wanadamu wanawaabudu viumbe waishio mbinguni kwani viumbe hao wamewaahidi mambo mazuri, wengine wakiahidiwa kupewa uzima wa milele, wengine kwenda mbinguni, wengine wanaabudu kwa majina wakina Mikael, sijui Gabriel, na Yesu ambao kimsingi hao sio Mungu.

Bali wao wamekuja kuwafanya wanadamu kama mateka, kama vile huku duniani nchi moja inavyoenda kutawala nchi zingine, tunaita Ukoloni na sasa Ukoloni mamboleo. Ndivyo na viumbe wa Mbinguni walivyofanikiwa kuwatalawa viumbe wa duniani yaani sisi wanadamu.

Wanadamu wanawaona malaika ni bora kuliko binadamu. Wanapaona Mbinguni ni bora kuliko duniani.

Ninachotaka kusema ni kuwa, mwanadamu alikuwa mkamilifu kabisa kabla hajakutana na hila za viumbe wa mbinguni, si ajabu hata Edeni ilikuwa hila za hao viumbe kwani wamejaliwa nguvu, uweza, akili na mamlaka ya kusema kitu kikawa.

Matatizo ya duniani hayataisha leo lakini atakayeyamaliza ni mwanadamu mwenyewe. Pale Mwanadamu atakapoacha kuwatumikia Viumbe wa mbinguni iwe ni malaika au mashetani ndio siku hiyo hiyo dunia hii itakombolewa.

Naamini, miaka ya hivi karibuni mwanadamu ataweza kukikabili kifo. Watu hawatakufa tena kutokana na matokeo ya kisayansi na tekonolojia. Kifo kitadhibitiwa.

Nafahamu kuwa kifo ilikuwa ni Mradi wa viumbe wa Mbinguni kumtawala mwanadamu. Lakini baada ya kifo kukidhibiti mamlaka ya mwanadamu itarejea kama ilivyomwanzo.

Kifo hakitadhibitiwa kwa kutamani kwenda Mbinguni. Watu wanachoshindwa kuelewa ni kuwa Kifo kimeletwa na viumbe hao hao wa mbinguni.

Sijajua Mungu yupo wapi kwa sasa, licha kuwa mahali popote yupo. Lakini hawezi ingilia mambo haya, mpaka siku ya hukumu.

Siku ya hukumu itafika pale ambapo Mwanadamu ataweza kukidhibiti Kifo.

Mbinguni sio salama kama watu wanavyofikiri.

Taikon nimemaliza, Leo sitaki maswali.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Unguja
...Umeruhusu Mawazo Yako kuona Halali kwenye Haramu. Pole
 
Back
Top Bottom