Hiyo title tu "Mbinu za kumdhibiti...." nilijua kuwa hapa nitapingana nawe. Kwa nini umdhibiti. Ikiwa unampenda, anakupenda - mnapendana - tena kudhibitiana kuna haja gani?
kijakazi na bili zote nalipa, nina kazi na sijawahi kufilisika na ninakupenda mno....................lol kweli huna shukrani
Kwanza hapa waombe samahani dada wanaosaidia kazi za nyumbani. Hilo jina lilishaacha kutumiak enzi za utumwa
hivi kipipi unakana ya kuwa kiu yako ni mumeo akupende na akujali? Atawezaje kukupenda kama anakutegemea...........??????? Be real............ furaha ya mwanumme ni kujitegemea na mwanaume yeyote anayemtegemea mwanamke hana furaha maishani mwake kwa sababu anapingana na nature aliyopangiwa na Mwenyezi Mungu.........
Napinga hiyo red kwani kwa mawaz yangu ni kuwa "furaha ya ndoa ni kutegemeana". Ahadi zenu zilikuwa "kukaa naye kwa raha na shida, uzima na ugonjwa...mpaka kifo kitakapowatenganisha". Ikiwa mwanamme "must" kutomtegemea mwanamke hata ikiwa wakati wa shida na ugonjwa, hiyo ahadi ingesomeka vyema kama ingekuwa "kukaa naye kwa raha na uzima...mpaka
shida na ugonjwa utakapowatenganisha."
.a real man hujiandaa kubeba majukumu yake tangia akiwa mdogo ............@King'asti
Kwenye familia yangu tangu wadogo, wanaume na wanawake tulifunzwa kufanyakzi na kusaidiana katika mtindo wa
hukutwanga huli, haikuwekwa kutafuta na kuchanja kuni, kutwanga na kukosha vyombo ni jukumu la msichana. Hata msichana alipoumwa au kutokuwepo, wavulana tuliingia jikoni. Leo niko mkubwa, kamwe sitokka na njaa au kula nje kwa kusubiri mke aje kunipikia.
Aidha, tulipokuwa JKT, wasichana na wavulana tulishirikiana kwa kila kitu, iweje leo nibadilike kwa sababu nimeoa. Kwanza huu msamiati wa kuoa/kuolewa haupo kwangu, ni KUOANA kwa maana ya kukubaliana.
Nambari 9 tayari imeshapata msemaji. Kama ni kweli ulivyoitetea baadaye, isahihshe, ondoa neno
hadharani kwani linakupa ruhusa ya kumpiga na kumnyanyasa faraghani.
Mimi wangu nitamsaidia kwa yote uliyosema nisitie mkono. Na hata hilo la ujauzito ambalo kweli ndio nature (mengine yote tunajipangia hakupanga Muumba), akijifungua ninamsaidia malezi ikiwemo kuadilisha mtoto nepi, kufua mikojo na mavi. Kamwe sitomwamsha dada wa kazi amshughulikie mtoto usiku, na mkewangu ndio kabisaaaaa, alishachukua jukumu nilisiloweza kulibeba mimi wakati wa ujauzito, kwa hivyo kumbebesha mengine nikiwa na mikono miwili...hapo nitakubali majirani waseme. I'll do it for the sake of my kids, for the sake of my lifemate.