Mbinu 10 zinazotumiwa na CCM kulinda madaraka

Richard Robert

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
632
Reaction score
340
1. Kesi za kubumba kama vile ugaidi, uhaini, kukamatwa na madawa ya kulevya, uhujumu uchumi n.k.
2. Kufunga watu bila kesi zenye mashiko (detention without trial - kumbuka mashehe wa Zanzibar);
3. Makosa ya mtandaoni na faini kubwa kubwa. TCRA ni agent wao mkubwa wa ukandamizaji.
4. Kutangaza watu si raia ili washindwe kuendelea kupigania haki;
5. Kuwanyang'anya leseni za biashara mawakili na kuwabambikiza kodi kubwa wafanya biashara;
6. Kuzuia mikutano, makongamano na maandamano kinyume na katiba. Wakati mwingine watu huambiwa wazi wakiandamana watavunjwa miguu au kuuliwa
7. Kutisha viongozi wa vyama kupitia ofisi ya msajili wa vyama na IGP
8. Kutumia ugaidi wa dola na uhalifu unaofadhiliwa na dola
9. Kutumia tume isiyo huru na kuing'ang'ania iendelee kusimamia uchaguzi
10. Kutetea katiba ya mwaka 1977 ili waendelee kuchakachua matokeo kupitia mamlaka makubwa ya rais.
 
Mbinu pendwa kupita zote🤡🤡🤡
8860003675.jpg
 
Wee unadhan huo udhaifu wa Wapinzani wamezaliwa nao ? Usione vinaelea…

Upinzani ulianzishwa na Magwiji kina Mabere Nyaucho Marando…kawaulize wakubwa zako huyo ni nani?

Mara kadhaa Mabalozi na vi NGO vyao walijaribu kukusanya Wapinzani na kuanza kuwapa Capacity building ya kuitoa Ccm baadae sana wanakuja kujua kumbe walikuwa wanatoa Training kwa 'Wapinzani' toka Kijitonyama

Hizo ndio mbinu za CCM kirefu chake Cham cha Mapinduzi

Hii nayo ni mbinu ya CCM? au husomi ukaelewa?
 
11) udhaifu, Tamaa na kukosa sera kwa wanaoitwa Wapinzani
... hivi mnaposema tamaa huwa mnamaanisha nini? Kwamba ndani ya upinzani wanajitokeza watia nia zaidi ya 30 wenye tamaa ya madaraka au? Au (wapinzani) wanateka, kujeruhi, na hata kuuwa wengine kwa sababu ya tamaa ya madaraka ama kuyalinda au kuyatafuta? Wapinzani wana tamaa!

Fisi kabeba mzoga anakimbia nao ili wenye tamaa (kwa akili yake) wasije wakamnyang'anya mzoga wake! Hivi mwenye tamaa hapo ni yupi? Anayekimbia na mzoga au wale wa kufikirika akilini mwake kwamba wakija watamnyang'anya mzoga? Mwenye tamaa ni yule aliyekwisha kula akavimbiwa, anatoa ushuzi ovyo, na kudharau waliompa madaraka lakini bado anang'ang'ania madaraka kwa nguvu zote au ni yule ambaye hata hayo madaraka hajui yanafananaje?
 
Tamaa ni kuacha Ukatibu Mkuu wa Taifa wa Chama chako na kuwa Balozi

Tamaa ni kukana msimamo wenu wa kumpa Ugombea Urais mtu mliekuwa mnamuita Fisadi

Tamaa ni kutangaza kususia uchaguzi wa Serikal za mitaa kwa kuwa si huru lakin mkaja kushiriki uchaguzi Mkuu wakati hakuna lolote lililoboreshw

Unahitaji mifano zaid ya Tamaa? Hapo sijaongelea Makamanda wa Covid 19 waliposaliti msimamo wa chama
... hivi mnaposema tamaa huwa mnamaanisha nini? Kwamba ndani ya upinzani wanajitokeza watia nia zaidi ya 30 wenye tamaa ya madaraka au? Au (wapinzani) wanateka, kujeruhi, na hata kuuwa wengine kwa sababu ya tamaa ya madaraka ama kuyalinda au kuyatafuta? Wapinzani wana tamaa!

Fisi kabeba mzoga anakimbia nao ili wenye tamaa (kwa akili yake) wasije wakamnyang'anya mzoga wake! Hivi mwenye tamaa hapo ni yupi? Anayekimbia na mzoga au wale wa kufikirika akilini mwake kwamba wakija watamnyang'anya mzoga? Mwenye tamaa ni yule aliyekwisha kula akavimbiwa, anatoa ushuzi ovyo, na kudharau waliompa madaraka lakini bado anang'ang'ania madaraka kwa nguvu zote au ni yule ambaye hata hayo madaraka hajui yanafananaje?
 
1. Kesi za kubumba kama vile ugaidi, uhaini, kukamatwa na madawa ya kulevya, uhujumu uchumi n.k.
2. Kufunga watu bila kesi zenye mashiko (detention without trial - kumbuka mashehe wa Zanzibar);
3. Makosa ya mtandaoni na faini kubwa kubwa. TCRA ni agent wao mkubwa wa ukandamizaji.
4. Kutangaza watu si raia ili washindwe kuendelea kupigania haki;
5. Kuwanyang'anya leseni za biashara mawakili na kuwabambikiza kodi kubwa wafanya biashara;
6. Kuzuia mikutano, makongamano na maandamano kinyume na katiba. Wakati mwingine watu huambiwa wazi wakiandamana watavunjwa miguu au kuuliwa
7. Kutisha viongozi wa vyama kupitia ofisi ya msajili wa vyama na IGP
8. Kutumia ugaidi wa dola na uhalifu unaofadhiliwa na dola
9. Kutumia tume isiyo huru na kuing'ang'ania iendelee kusimamia uchaguzi
10. Kutetea katiba ya mwaka 1977 ili waendelee kuchakachua matokeo kupitia mamlaka makubwa ya rais.
Kiuhalisia sio mbinu za ccm. Ni mbinu za vyombo vya dola zikishirikiana na ccm. CCM kama CCM hawana ubavu huo.
 
Tamaa ni kuacha Ukatibu Mkuu wa Taifa wa Chama chako na kuwa Balozi

Tamaa ni kukana msimamo wenu wa kumpa Ugombea Urais mtu mliekuwa mnamuita Fisadi

Tamaa ni kutangaza kususia uchaguzi wa Serikal za mitaa kwa kuwa si huru lakin mkaja kushiriki uchaguzi Mkuu wakati hakuna lolote lililoboreshw

Unahitaji mifano zaid ya Tamaa? Hapo sijaongelea Makamanda wa Covid 19 waliposaliti msimamo wa chama
Tamaa ya madaraka ilimwondoa magufuli duniani.
 
Back
Top Bottom