SoC01 Mbinu bora na Maridhawa kwa Kuinua Maisha ya Watanzania kufikia mwaka 2040

SoC01 Mbinu bora na Maridhawa kwa Kuinua Maisha ya Watanzania kufikia mwaka 2040

Stories of Change - 2021 Competition

silver jerry

Member
Joined
Mar 24, 2017
Posts
12
Reaction score
9
Watanzania wengi wanasumbuliwa Sana na ukombozi wa kifikra, Changamoto nyingi Sana za Maisha zinaielemea Jamii kwa sababu ya Elimu Mbovu na Mijiundo ya kiutawala tuliorithi kwa wakoloni! Hii imekua ni dhana mbovu Sana katika kuikwamua jamii katika lindi la umasikini wa fikra, mitazamo na Maisha.

Yafuatayo yanapaswa kufanyika haraka Sana katika kurudisha Nuru ya Maisha yamafanikio na Mitazamo kwa Watanzania:

1. Kuanzishwa kwa Somo la Siasa kwa Elimu ya Tanzania, Ndani ya mtaala wa Elimu ya Tanzania kuanzia Elimu ya Msingi ,Sekondari ,na Chuo , somo la Siasa linatakiwa kua Ni lazima lisomwe na Kila mwanafunzi na liwe Ni lazima

Hii itasaidia Sana katika Kuinua ufahamu wa Watu wake mpaka kufikia Mwaka 2040 , watu watajua Maisha yetu sote n Siasa na wataacha kurubuniwa na watawala maana somo la Siasa limewakomboa na kufanya wajue nini Na namna gani tutaendesha Maisha yetu na nchi yetu kiujumla.

2. Kubadili Muundo wa Kupata Askari wetu (Polisi) , kuna tatizo Sana katika nchi yetu hasa katika suala la utoaji haki na kifatilia kesi na hatima za madai , hivo sheria za kuwapata polisi zinatakiwa kubadilishwa ,na pia Muda wamafunzo unatakiwa kubadilishwa toka miezi 9 mpaka miaka 3 ya masomo.

Pia wanatakiwa waweke Utaratibu wa kumfundisha Polisi somo la sheria angalau atoke na Diploma ya sheria ya chuo kinachotambulika na serikali. Hili litasaidia kupatikana kwa haki zawatu na kuimarisha utu; Kutapunguza Lindi na wingu la Polisi kua na tuhuma za mara kwamara zakutumika na Serikali iliyoko madarakani kwa maslahi yao binafsi na sio Taifa letu Tanzania.

3. Kuanzishwa kwa vyuo vya Kati Vingi takribani kimoja katika kila Wilaya.Katika mitaala yetu ya Elimu ,tunapaswa kuwa na Vyuo vikuu vichache Sana vitavyopata watalaam Competitive wataosaidia kusimamia walioko chini yao katika kuijenga nchi , Vyuo vyakati vitatoa technician wengi stable wataokua wanasiadiwa kwaukaribu na hao wataaalam wajuu , sasa hivi ni tofauti nchi yetu inawatu wenye madegree wengi ila nihopeless na useless kwa Taifa, Tunataikiwa kuiga mifumo yachina katika kuinua viwanda na uchumi.

4. Wafungwa wanatakiwa kutumika kuzalisha Mali na Kuinua taaluma zao, hii itasaidia kukuza uelewa wao ,pindi watapomaliza Mafunzo yao katika namna yaadhabu au kizuizi wapewe asilimia 10% yawalichokizalisha wakiwa Jela, itawasaidia Kupata mitaji nakurejea mitaani wakiwa na nidhamu, mitaji na ari yakuishi kwakuzifata sheria za jamhuri.
Kuachana na dhana ya kupewa msamaha na kurudi mtaani pasipokua na kitu mwisho kurudia makosa na kurudi jela.

5. Uzalendo sio kuisifu serikali kwa kila kitu, elimu yakweli yauzalendo itolewe pasipo kuchakachuliwa kwamanufaa yanchi yetu.

Mwisho Mungu ibariki Tanzania
 
Upvote 0
Back
Top Bottom