SoC01 Mbinu bora za kujikomboa kiuchumi na kibiashara

SoC01 Mbinu bora za kujikomboa kiuchumi na kibiashara

Stories of Change - 2021 Competition

strong star

Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
36
Reaction score
42
Moja kati ya vitu muhimu sana katika kuinua uchumi wa nchi pamoja na kuleta maendeleo kuanzia kwa mtu mmoja mmoja adi kwa taifa ni biashara, kuna biashara za aina nyingi nyingi kama vile maduka ya vyakula, magenge, na kadhalika.
Kila biashara unayoiona, kuijua au kuimiliki usije kamwe ukaidharau kwani ina changia kwa kiasi kikubwa mzunguko wa pesa na pato la taifa.

Leo tunaenda kuona mbinu bora za kukuza biashara na kujiinua kiuchumi na maendeleo.

*Uthubutu na kujiamini.
Unapaswa kwanza kujiamini kwamba unaweza na utafanikiwa kwa asilimia mia moja, kisha uwe na moyo wa uthubutu na sio KUJARIBU kama wanavyo fanya watu wengi, kwani ukiwa unajalibu jalibu tu ata ikija changamoto ndogo tu unaacha kabisa biashara na kusema NILIJALIBU TU,kisha kuingia kwingine mwisho kukata tamaa kabisa na biashara wakati wengine wanafanikiwa.

*Kujali na kuthamini.
Unatakiwa kujali na kuthamini kila hatua, ushindani wa biashara, wateja, pia kila changamoto inayojitokeza mbele ata kama ni ndogo sana kwani ukiweka dhalau itaweza kukuangusha chini au kukukwamisha mahali.

*Kujitoa na kujituma.
Lazima ukubali kujitoa zaidi na pia kujituma katika biashara yako , Kwa kuwa hizo ndizo nguzo za mafanikio ata kama kuna changamoto au ushindani piga moyo konde,sukuma zaidi kisha songa mbele utafanikiwa tu ata kama isiwe leo basi ni kesho.

*Malengo na misimamo.
Lazima ujiwekee malengo na kuyatimiza, ujiwekee misimamo yako na miiko yako hasa kwenye biashara yako kwani unaishi na jamii na ndani yake kuna watu tofauti tofauti, hivyo hakikisha unasimamia miiko na misimamo yako.

*Kubali kushauliwa na kukosolewa.
Pokea kila ushauri kisha tafakali kwa akili yako unayoyaona yanafaa chukua fanyia kazi yasiyo faa tupa pembeni songa mbele, Siku zote jiandae kukosolewa au kusemwa vibaya kwani kamwe hautaweza kuwalidhisha wote katika jamii ata ufanyaje.

*Ucheshi na uchangamfu.
Hakikisha unakuwa mcheshi na mchangamfu kwa wateja wako kila siku ata kama sio tabia yako au una matatizo yako mengine, Ikiwa biashara yako ni ya vyakula basi buni ata michezo mbali mbali kama vile bao,drafti, na mingine, ili tu kuwavuta zaidi wateja wako.

*Ubunifu, uzalendo na uhakika.
Unapaswa kubuni mbinu mpya kila uchao ili kuvutia wateja wako na wapya, pia uhakika wa huduma zako kila mteja atakapoitaji viwepo na ikibidi zingatia sana mida yako ya kufunga na kufungua ( epuka dhalula zisizo na ulazima ) ili kuweka uzalendo katika biashara yako.

*Usiri na uaminifu.
Unapaswa kuweka kumbukumbu kila siku na kila kitu kwani Mali bila daftali uisha bila habari, hakikisha kuna usiri wa mwenendo wa biashara yako pia unatakiwa kuwa mwaminifu kuanzia wewe, biashara yako mpaka kwa wateja wako.

*Mshilikishe Mungu mwenyezi.
Kwa imani yako unapaswa kumshirikisha Mungu wako katika biashara yako na kujiepusha na imani za kishilikina na imani zingine zisizo faa.

Hakika kwa hayo yakifanyiwa kazi kisawasawa katika biashara yako ,Mpendwa utafanikiwa tu na kujikomboa kiuchumi na kujiletea maendeleo. KUMBUKA usidhalau kazi yoyote na HIZO unaziona wewe ndogo watu ndio ufanikiwa bazo.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom