Mbinu gani ya kuzuia Nyoka wasiingie nyumbani au wasisogee karibu na nyumba? Kuna dawa yoyote ya kufukuza?

Kuna miti inatoa harufu inayowafukuza
 
Hilo pori unalokaa ngoja tuje kuchimba madini hao nyoka wataondoka.
 
Mwaga oil chafu ama mafuta ya taa, kuna aina ya majani ukipanda kuzunguka nyumba hawatosogea kabisa nafikiri ni kama UKOKA fulani hivi yanakatakata, nyoka hapendi kupita pita mule.
Pia kuna mchai chai(lemongrass) nao ni mzuri
Ukipata Epsom salt(magnesium sulphate) inasaidia.
Harufu za mdalasini, clove nazo ni repellent kwa mjomba snake.
 
Fuga kuku wa kienyeji na paka wataifanya kazi hiyo bila wewe kujua.
 
Panda Mchaichai kuzunguka nyumba kama hakuna Fensi

Choma Tairi la Gari au Pikipiki au Baiskeli walau Mara moja kwa mwezi hawapendi ile harufu wanaikimbia


Mwaga Oil chafu kuzunguka nyumba, wengine wameshauri ichanganywe na diesel, au Mafuta taa, au petroli.

Mwaga chumvi malangoni pako, hakuna nyoka atakatiza hapo.
 
Nlikua nasubiri hii comment nafikir hii ndo njia rahisi zaidi
 
Mwaga oil chafu kuzunguka nyumba.Hii ni zaidi ya sumu mkuu.
 
Otesha michaichai karibu na mlangoni. Katika harufu nyoka hapendi ni ya Mchaichai (Lemon grass)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…