Mbinu gani ya kuzuia Nyoka wasiingie nyumbani au wasisogee karibu na nyumba? Kuna dawa yoyote ya kufukuza?

Wakuu, leo nilikua nimelala chini ndan chumbani. Kushtuka naona nyoka mdogo karibu na kichwa changu ikabidi nimuue.

Lakin pia kijana ashawai ua nyoka kama wawili mlangoni mwingine upenuni.

Nipeni mbinu za kupambana na hawa viumbe ziwe zamwanzo nilijiapiza asili za jadi au za kisa sa!!
Umevamia makazi yao.
Hapo hakikisha mazingira yanayokuzunguka hayana vichaka ama nyasi kubwa
 
Mkuu kwa ushauri murua kabisa panda hii bustani nyumbani kwako ikishakuwepo hii bustani nyoka hawasogei hapo
Hii bustani pia inazalisha oxygen nyingi sanaaa kwaio unaweza kuweka hata sebuleni kwako
 
Attachments

  • 20240720_073634.jpg
    20240720_073634.jpg
    1.3 MB · Views: 16
Mkuu kwa ushauri murua kabisa panda hii bustani nyumbani kwako ikishakuwepo hii bustani nyoka hawasogei hapo
Hii bustani pia inazalisha oxygen nyingi sanaaa kwaio unaweza kuweka hata sebuleni kwako
Snake Plant, lakini hata huu Marigolds pia unasaidia, hawapendi harufu yake.

Hakikisha mazingira ya kuzunguka nyumba yako ni masafi kila siku, yasiwe na nyasi ndefu, vichaka ama matakataka yasio na mpangalio kwa sababu nyoka chakula chake kikubwa ni panya. Hivyo kama ndani kwako ni kuchafu maana yake kuna panya 🤣 wengi hivyo tegemeea sana nyoka kuwa mgeni wako kila siku kukutembelea.
marigolds.jpg
 
ila chumvi ni kiboko ya nyoka. Aliwahi kuingia jikoni nyoka mkubwa tu nikamzungushia chumvi nikamwambia tulia hapo hapo, nyoka hakufurukuta nikaenda kuita mtu anayeweza kuuwa nyoka tukakuta ametulia palepale, chumvi imemdhibiti.

Wanaosema kuna majani kama ukoka yanawazuia nyoka sijui sio kweli, kwangu yapo na wanapita humo humo spidi tu, wala tiles pia haziwazuii, wanatambaa vizuri tu.

Mtoa uzi jitahidi kuhakikisha ndani ya nyumba kakuna panya. Usiache milango/madirisha wazi hata mchana. Pia kama milango ina gaps kwa chini hakikisha unaziba
 
Ni nini hasa usababisha chumvi kumdhibiti nyoka?
 
Back
Top Bottom