Qchicksolution
Member
- Aug 22, 2017
- 11
- 22
Sote tunafuga kuku ili kupata mayai au nyama kutoka kwa kuku hao,lakini mtafaruku hutokea pale kuku hao wanapoacha kula chakula na kuamua kulana wao kwa wao au kula mayai kabisa.kama ulishawahi kufuga kuku wengi utanielewa vizuri maana kuna uwezekano mkubwa ukawa umeshasumbuliwa sana na tabia hii mbaya ya kuku.
baada ya kusumbuliwa sana na hii tabia niligundua kuwa tabia hii husababishwa na mambo mengi ikiwamo kuku kubanana kiasi cha kuwasababishia stress,lishe mbaya sanasana upungufu wa vitamin D na Calsium,pamoja koo tata za kuku(kuna kuku wengine hata ufanyaje yani wanapenda shari mwanzo mwisho)
Mara yangu ya kwanza kabisa kuona tatizo lilianzia wakati vifaranga bado wadogo kabisa(Wiki tatu) nikaanza kuona michezo hiyo..ambayo waliendelea nayo kadiri walivyokuwa wakubwa,mwanzo sikustuka hadi pale nilipokuta mmoja amekufa na kukuta ametobolewa sehemu ya nyuma yote imejaa damu na bado wanaendelea kudonoa!ushauri wa kwanza nilioupata toka kwa daktari wa mifugo ni kuwapa kuku hao chakula chenye calsium kwa wingi na majani ,nikawachanganyia chakula na chokaa pamoja na mifupa lakini bado kudonoana kulikuwa pale pale.
baada ya kushauriana na baadhi ya wafugaji nikapata wazo la kuwakata midomo (debeaking) hii ilipunguza kwa kuwa walikuwa wanashindwa kudonoa vizuri lakini waliendelea kudonoana hivyo hivyo hadi kupelekea wengine kukosa manyoya kabisa.
kwa upande wa kuku wanaokula mayai nikashauriwa ni toboe mayai kadhaa na kuyajaza pilipili ili waogope kudonoa baada ya kupata ladha hiyo.mbinu hii nayo haikufua dafu maana walikuwa wanaonja wakiona pilipili wanaliacha wanatafuta mengine!!
baada ya kuhangaika hivyo nikaamua kuegemea zaidi kwenye lishe bila kutegemea ushauri wa madaktari wa mifugo wala wafugaji wengine,hapa nikagundua kuwa mifupa ya samaki wa baharini na shells zao ndio wanaongoza kwa kuwa na calsium nyingi about 40%,wakifuatiwa na chokaa 38%, DCP 23%, mifupa 20%.kutokana na upatikanaji mgumu wa hivyo vya baharini nikaamua niegemee kwenye chokaa,ambapo katika mfuko wa chakula wa kg 50 nikawa naongeza chokaa hadi ilafikia kilo 5 kwa mfugo mmoja wa chakula lakini bado haikufua dafu!!
LASTLY!
mara nyingine sio kila tatizo katika ufugaji linawezakutatuliwa kupitia mambo yanayoandikwa kwenye madaftari(literatures),kwakuwa uhalisia unaweza kuwa ni kitu kingine tofauti kabisa.Binafsi baada ya kuhangaika sana mwisho wa siku nikagundua kuwa nikiwapa chokaa kuku wangu kila asubuhi kabla ya kuwapa chochote,na chokaa hiyo nisichanganye na kitu chochote ndio tiba halisi ya tatizo hili na sikuwahi kuiona tena tabia hii haijalishi nimewapa pumba tu au sijawapa chochote.inaonekana labda chokaa inayouzwa haina calcium content kubwa au inapochanganywa na chakula mchanganyiko wako unakuwa sio uniform! hapo bado sijaelewa,lakini kwa sasa nnachojua ni kuwapa chokaa kidogo asubuhi kabla ya mambe mengine.angalizo ni kwamba ili calsium au phosphorus ifanye kazi kwa kuku inahitaji vitamin D ambayo inapatikana kwenye premix zinazouzwa maduka ya mifugo au kutoka kwenye miale ya jua.mimi nawatoa nje wapigwe na jua ili waweze kuabsorb vitamin D.