SoC04 Mbinu kwa ajili ya kuboresha Sekta ya Uchukuzi

SoC04 Mbinu kwa ajili ya kuboresha Sekta ya Uchukuzi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Elipa malipo

Member
Joined
May 27, 2024
Posts
7
Reaction score
4
Moja - Itengwe bajeti ya kutosha katika sekta hii; zitolewe fedha ambazo zitakidhi mahitaji ya sekta ya (UCHUKUZI), hata kama sio kwa asiilimia mia moja. Hii itasaidia miradi mfano reli,barabara,maji n.k kukamilika tena kwa wakati na uchumi wa watu na taifa utakuwa.

Mbili - Kuwapa kazi ya ujenzi wa miradi mbalimbali mfano, miradi ya maji, umeme, Barabara n.k. Wakandarasi wachapakazi na kuwasimamia kwa ukaribu zaidi. Hii ni pamoja na kusaini mikataba inayowabana, endapo wakiaribu kazi walipe fidia kubwa ili wajenge kwa kiwango kikubwa. Kinachokizi vigezo.

Tatu - Serikali iweke waziri ambaye atasimamia haki, ambaye atahakikisha viongozi wengine walio chini yake wanachapa kazi na wanakuwa na matumizi bora ya fedha na ambao ni wakali pale mambo yanapoenda kinyume, hao watumishi wawe ni wazalendo mfano, Makame Mbarawa pia Serikali ishirikiane vya kutosha ili haweze kukamilisha hili.

Nne - Kuwawajibisha au kuwafuta kazi kabisa viongozi wasio waadilifu; hao ni viongozi wapenda rushwa, wazembe, waongo na wasio penda haki kwa hiyo wawajibishwe au wafutwe kazi kabisa. Hii itakuwa ni fundisho kwa viongozi na watu wenye tabia sawa na hizi. Itapelekea viongozi kuwa makini na kufanya kazi kwa bidii.

Tano - Kupunguza matumizi; Hii itasaidia bajeti ya serikali kuwa kubwa na yenye manufaa kwa wananchi. Miradi mingi itakamilika na kupelekea serikali kukusanya Kodi za kutosha kwa ajili ya miradi mbalimbali mfano, maji, Barabara, reli n.k. Matumizi mengine hayazalishi badala yake yanapoteza. Ili miradi iendele kujengwa inabidii ile fedha izalishe.

Sita - Kutumia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii: ili wananchi wafahamu hali ya maendeleo ya miradi na kutoa maoni mbalimbali; vyombo hivyo ni chombo cha Taifa Cha Utangazaji(TBC) na mitandao ya kijamii mfano Jamii Forums.

Saba - Serikali ijenge miradi ya kisasa ambayo inaenda na Dunia ya sasa; Inahitaji kujenga miradi ya kisasa ili kuchochea ufanisi. Kuna miradi mingine ilishapitwa na wakati kabisa, kwa hiyo ijengwee . Kwa Sasa Dunia ina mapinduzi makubwa ya kitechnolojia yanayochochea maendeleo mfano reli ya kisasa (SGR) kutoka jinini Dar salaam mpaka Makotopola jijini Dodoma. Ujenzi wake ni rahisi kuliko ile miradi ya reli ya kizamani. Ya (TAZARA)

Nane - Kuboresha sekta ya elimu; ambayo inafanya kazi kwa ukaribu na sekta ya uchukuzi. Hii itasaidia kupata watalaam ambao ni bora katika ujenzi bora wa miundombinu ya kisasa, Sekta hii iboreshwe kwa kuongeza vifaa vya kufundishia pamoja na walimu. Vfaa mfano,vitabu vya kisasa na pia mwanafunzi huyo hasome kwa vitendo. Walimu wachapakazi,waaminifu na wenye lengo la kujenga taifa bora. Chanzo cha waandisi bora ni elimu,hivyo iboreshwe ili elimu iwasadie waandisi wajenge miradi mfano,reli,madaraja,umeme n.k.

Tisa - Serikali ihakikishe inawasimamia; wawakilishi wa majimbo ambao ni wabunge kwa ukaribu ili kuhakikisha wanafikisha changamoto za wananchi bungeni kwa wakati. Kwasababu miradi ipo majimboni ambapo mbunge anahusika. Ikiwa Kuna changamoto katika mradi fulani, serikali itapata taarifa mapema na kulifanya kazi suala hilo kwa wakati pia wafanyakazi au watumishi katika sekta hiyo ya (UCHUKUZI ) walipwe kwa wakati Kwa kufanya hivi itapelekea huduma mbalimbali kutoka Kwenye sekta hii kuwa bora mfano,usafiri wa nchi kavu yaani barabara,reli n.k.

Kumi - Kuhakiki miradi kabla ya kuanza matumizi; miradi mingine inaweza kuwa ni mibovu,yaani haijakizi vigezo lakini ikalusiwa kuanza kutumika. Mradi ambao umejengwa haukukizi vigezo kwanza, hautadumu pili, utapelekea sekta husika na serikali kwa ujumla kupata hasara mfano, miradi ambayo inakaa muda mfupi na wakati imetumia mamilioni ya fedha ndio sababu mojawapo ya miradi kukwama na kutokamilika kwa wakati au kutokamilika kabisa. Mfano, miradi ya maji iliyokuwa imekwama kwa muda mrefu.

Kumi - Zitungwe sheria ambazo zitakuwa zinawataka viongozi na wananchi kwa ujumla kufanya kazi kwa bidii na Kwa ufanisi mfano, kiongozi ambaye atakuwa anevunja hiyo sheria. Atolewe madaraka ili iwe funzo kwa wengine wanaofanya vitendo sawa na hivyo. Ila kwa upande wa afrika kwa maoni yangu napo miundo mbinu mingi ni mibovu mfano, katika nchi ya Uganda, Congo Burundi n.k. lakini kwa Tanzania tunaweza na kukawa na tofauti kabisa. Ulaya nao walikuwaga sawa na sisi miaka mingi iliyopita lakini kwa Sasa ni matajiri wakubwa kwa sababu wanasheri zinazolinda miradi yao ya kimaendeleo.

Kwa ujumla serikali inabidii kuwekeza zaidi katika sekta ya uchukuzi( miundombinu) lakini pia katika sekta nyingine zinazosaidia sekta hii mfano, sekta ya elimu kwa kiasi fulani. Kwa nyanja kuu tatu, moja Kiakili, mbiliki jamii na tatu kiuchumi.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom