Elipa malipo
Member
- May 27, 2024
- 7
- 4
Hii ni sekta ya muhimu katika uchumi wetu. Ikiwa usimamizi wa sekta hii utaendelea kusimamiwa vizuri uchumi wetu utapanda kwa miaka mitano (5),kumi (10) na kuendelea.katika sekta hii tunapata malighafi mbalimbali kwa ajili ya viwanda mbalimbali mfano, alizeti kwa ajili ya kutengeneza mafuta ,miwa kwa ajili ya sukari,pamba kwa ajili ya kutengeneza nguo,pareto kwa ajili ya kutengeneza dawa ya mbu n.k.
Hapo tunapata kutoka katika mazao ya mashambani. Ufugaji tunapata maziwa,nyama n.k. katika UVUVI tunapata samaki ambao ni chakula bora kwa afya ya mwanadamu(protini)
Zifuatazo ni mbinu kwa ajili ya kuboresha sekta ya ufugaji ,kilimo na uvuvi
Moja,kujenga na kuboresha mabwawa mbalimbali yanayozalisha maji kwa ajili ya sekta hiyo mfano, bwawa la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililopo mkoani Morogoro ambalo linasaidia katika kilimo cha mpunga mkoani humo.Hii itasaidia pia ongezeko la upatikanaji wa zao hilo kwa sababu kilimo cha umwagiliaji kinaweza kikatumia misimu miwili kwa mwaka mmoja mfano, nchini China wanaoongoza kwa uzalishaji wa zao hilo dunianikwa sababu ya kutumia kilimo cha kisasa kinachohusisha umwagiliaji.
Mabwawa hayo pia yatasababisha gharama za mazao kushuka bei kwa sababu uzalishaji utakuwa mkubwa na wa kisasa mfano, wa mazao mengine ni miwa,alizeti,mtama,ufuta n.k.
Mbili.Vijengwe viwanda mbalimbali
vya kuchakata malighafi mbalimbali nchini zitokanazo na ufugaji; mfano, mifugo ya ng,ombe endapo itafugwa kwa mbinu bora na za kisasa itasaidia na wafugaji wengi watanufaika. Ngombe ana faida nyingi moja upatikaji wa maziwa, mbili nyama n.k. Ujenzi wa viwanda utasaidia katika upandishaji thamani
wa bidhaa. Zitakazokuwa zinazalishwa na kusababisha wananchi wengi kupata bidhaa ambazo zitachukuwa muda mrefu mpaka kufikia muda wake wa kuharibika pia, bei za bidhaa zitashuka na wananchi wengi watanufaika.
Tatu.Kuboresha miundo mbinu ya usafiri; mfano, wa miundombinu hii ni barabara mbalimbali bora na za kisasa.Barabara hizi zitasaidia kusafirisha mazao na mifugo mbalimbali kutoka maeneo zinapopatikana mpaka viwandani,kwa ajili ya kuchakatwa na kutengeneza bidhaa mbalimbali mfano,miwa ambayo ikichakatwa viwandani itapunguza uhaba wa sukari nchini na kupelekea maisha ya watu kukua na gharama zake kushuka.Uwepo wa miundo mbinu bora ya barabara itasaidia kuokoa muda.
Nne. Uwekezaji katika sekta hii; serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa sekta hii inapata fedha za kutosha.Fedha hizi zitasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta hii mfano,kutokuwa na zana za kisasa (magari ya kilimo) zinazotosheleza mahitaji, uhaba wa mvua kwa baadhi ya maeneo nchini mfano, mkoani Singida,Shinyanga na jijini Dodoma.
Tano.Wakulima nchini wapewe elmu ya kutosha kwa ajili ya kilimo cha kisasa chenye tija;wafahamu kuhusu majira mbalimbali katika mwaka. Maeneo ya equatorio ni maeneo yenye mvua ya kutosha, misitu mirefu n.k. Ni rafiki kwa kilimo cha kahawa,maparachichi,mbogamboga kwa sababu Kuna mvua za kutosha mfani, wa mikoa hiyo ni Mbeya,Katavi,Njombe n.k.
Sita.Uvuvi,sehemu hii serikali ihakikishe inasimamia uvuvi haramu ambao hunapelekea ukosekanaji wa samaki bora na pia idadi ya samaki kupungua .Hii inasababishwa na wavuvi haramu wanaovua bila kuwa na ruhusa na kibali cha kuvua samaki.wengi wanatumia dawa ambazo ni hatari kwa maisha ya viumbe hao.
Serikali ingetunga sheria Kali ambazo mvuvi akikutwa hana kibali kutoka kwa serikali na mamlaka huusika anavua.Hatozwe kwanzia millioni moja, na hafungwe jera, hiyo itakuwa ni adhabu tosha kwa muhusika.
Kwa ujumla; sekta hiyo inatakiwa kuboreshwa ili kuhakikisha malighafi mbalimbali zinapatikana nchini kwa gharama nafuu na Kwa ubora unaotakiwa mfano, sukari, mafuta ya kupikia,samaki wa kusindika wanokaa muda mrefu,maziwa, nyama n.k. Uchakataji utatokana na uboredhaji wa viwanda nchini kwa kufanya hivyo uchumi utakuwa na gharama za maisha zitashuka.

Upvote
1