MBINU MBALIMBALI ZA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UJENZI.

a sinner saved by Christ

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
611
Reaction score
993
Mbinu mbalimbali zinazoweza kutumika kupunguza /kuokoa gharama zisizo za lazima katika ujenzi.

1)MBADALA WA TANK LA KUHIFADHIA MAJI.
Naanza na hii ,maeneo yetu mengi maji yanatoka kwa mgao wa mara moja kwa juma hivyo utalazimika uhifadhi maji kwa ajili ya kazi yako ya ujenzi.
Njia hii ni kutengeneza mbadala wa tenki/karo ya kuhifadhia maji kwa ujazo unaotaka wewe lita 2000L,300L n.k
Mbinu ,unatumia tofali zako zilizopo site kwa ajili ya kazi ya ujenzi,unatumia kwa muda unazipanga kwa kuzilaza juu ya nyingie kutengeneza mfano wa kujenga kuta pande nne (mfano wa karo.) Halafu unalaza turubai water proof isiyoruhusu maji kupenya ikifunika sakafu ndani ya hizo kuta nne mpaka eneo la ndani ya hizo kuta nne ulizozitengeneza kwa kusimamiaha tofali tupu,bila kujengea na simenti na mchanga.

FAIDA
Utakuwa umeokoa kiasi kikubwa cha fedha wastani wa zaidi ya shilingi laki 5 , fedha ambayo ungetumia kwa kukodi au kununua mapipa au majaba au tenki (vyombo vikubwa vya kuhifadhia maji) lakini hapa utakuwa umetumia elfu 15 tu ya turubai,mana tofali utakazitumia ni baadhi ya sehemu ndogo ya zile zilizoko site kwako.

NAKARIBISHA MBINU NYINGINE zinazoweza kutumika kusaidia tunaoanza kujenga kwa kuunga unga masikini wenzangu,ku save gharama,kupunguza gharama zisizonza lazima kwenye hatua yoyote ya ujenzi.

picha chini-hapo amehifadhi kati wastani wa maji lita 2000-3000 kwa makadirio hapo angenunua tenk ni kati ya laki 3 mpaka 5 .
na hata kama angekodi gharama ingezidi hiyo 15,000 aliyotumia kununulia turubai.
Na hata kama angenunua mapipa au majaba bei ingezidi ,kwenye ujenzi hata ukisevu laki moja ni kubwa .
 
Attachments

  • IMG_20241021_113811_113.jpg
    IMG_20241021_113811_113.jpg
    596.7 KB · Views: 26
  • IMG_20241021_113749_674.jpg
    IMG_20241021_113749_674.jpg
    776.6 KB · Views: 24
  • IMG_20241021_113843_721.jpg
    IMG_20241021_113843_721.jpg
    581.8 KB · Views: 8
2) kujenga msingi kwa tofali inchi sita badala ya mawe kwa ardhi ya baadhi ya maeneo kama mkoa wa Dodoma,Singida ,Kibaha n.k kadiri ya uzoefu wangu.
3)kutokujenga mkanda wa lenta au zege juu ya msingi yaani baada ya kujenga msingi wa tofali za kulala ,inafuatia tofali za kusimama za ukuta directly moja kwa moja unaunga.
(inapunguza gharama ya nondo simenti ,kokoto,mchanga ,maji ambayo yangetumika kuweka zege kwenye msingi
 
Attachments

  • images - 2024-10-23T164153.871.jpeg
    images - 2024-10-23T164153.871.jpeg
    44.8 KB · Views: 10
2) kujenga msingi kwa tofali inchi sita badala ya mawe kwa ardhi ya baadhi ya maeneo kama mkoa wa Dodoma,Singida ,Kibaha n.k kadiri ya uzoefu wangu.
3)kutokujenga mkanda wa lenta au zege juu ya msingi yaani baada ya kujenga msingi wa tofali za kulala ,inafuatia tofali za kusimama za ukuta directly moja kwa moja unaunga.
(inapunguza gharama ya nondo simenti ,kokoto,mchanga ,maji ambayo yangetumika kuweka zege kwenye msingi
Hapa unaweza ukakuta nyumba imemeguka.
 
Hapa unaweza ukakuta nyumba imemeguka.
Kwa maeneo haya niliyoyataja singida,dodoma na kibaha naongea kwa uzoefu maana ndio sehemu nilizojenga vibanda.
ila nilishangaa dodoma kuona jamaa kajenga msingi tu wa nyumba ya kawaida ya vyumba vinne kwa gharama ya milioni 25?? BAJETI ya kujenga nyumba ikafika hatua ya kuingilika kibishi unahamia kabisa inabaki finishingi chache tu,mwingine anaimalizia kwwnye msingi tu..
tinatofautiana uwezo
25M imeishia kwwnye kiti cha msingi tu,wa nyumba ya kawaida tena siyo ghorofa?? nilishangaa sana ,nyumba ya mtu binafsi tena sio ya taasisi.
Kwa uimara ni kweli inakuwa imara mara dufu mana hiyo zege inayomwagwa hapo sio ya mchezo.

Ila mimi kwa uziefu wangu na umasikini wangu kwa mikoa hiyo (singida,dodoma,kibaha)nimejenga kimasikini misingi ya matifali inchi siti unalaza,bila zege /lenta ,unaunga tofali za kusimama,lenta zege inapita juu ya dirisha tu basi,na nyumba au vibanda vyangu havijawahi kuwa na changamoto ya nyufa.Naongea kwa uzoefu sio nadharia sio kwa kusikia.TENA na dodoma kuna matetemeko ya ardhi ila nyumba haihawahi kupata hitilafu au nyufa.

Kama JF ingekuwa na members masikini wenzangu kama mimi waliojenga kwa mfumo huu nao wangetoa ushuhuda wao ,ila bahati mbaya au nzuri JF ni ya matajiri.
 
Mbinu mbalimbali zinazoweza kutumika kupunguza /kuokoa gharama zisizo za lazima katika ujenzi.

1)MBADALA WA TANK LA KUHIFADHIA MAJI.
Naanza na hii ,maeneo yetu mengi maji yanatoka kwa mgao wa mara moja kwa juma hivyo utalazimika uhifadhi maji kwa ajili ya kazi yako ya ujenzi.
Njia hii ni kutengeneza mbadala wa tenki/karo ya kuhifadhia maji kwa ujazo unaotaka wewe lita 2000L,300L n.k
Mbinu ,unatumia tofali zako zilizopo site kwa ajili ya kazi ya ujenzi,unatumia kwa muda unazipanga kwa kuzilaza juu ya nyingie kutengeneza mfano wa kujenga kuta pande nne (mfano wa karo.) Halafu unalaza turubai water proof isiyoruhusu maji kupenya ikifunika sakafu ndani ya hizo kuta nne mpaka eneo la ndani ya hizo kuta nne ulizozitengeneza kwa kusimamiaha tofali tupu,bila kujengea na simenti na mchanga.

FAIDA
Utakuwa umeokoa kiasi kikubwa cha fedha wastani wa zaidi ya shilingi laki 5 , fedha ambayo ungetumia kwa kukodi au kununua mapipa au majaba au tenki (vyombo vikubwa vya kuhifadhia maji) lakini hapa utakuwa umetumia elfu 15 tu ya turubai,mana tofali utakazitumia ni baadhi ya sehemu ndogo ya zile zilizoko site kwako.

NAKARIBISHA MBINU NYINGINE zinazoweza kutumika kusaidia tunaoanza kujenga kwa kuunga unga masikini wenzangu,ku save gharama,kupunguza gharama zisizonza lazima kwenye hatua yoyote ya ujenzi.

picha chini-hapo amehifadhi kati wastani wa maji lita 2000-3000 kwa makadirio hapo angenunua tenk ni kati ya laki 3 mpaka 5 .
na hata kama angekodi gharama ingezidi hiyo 15,000 aliyotumia kununulia turubai.
Na hata kama angenunua mapipa au majaba bei ingezidi ,kwenye ujenzi hata ukisevu laki moja ni kubwa .
Nimeipenda hii
 
Back
Top Bottom