robbyr
Senior Member
- Apr 8, 2017
- 129
- 221
Zifuatazo ni Kanuni na Mbinu mhimu za kuishi na watu vizuri. Kanuni hizi nilizipata kwenye andiko la gazeti la Mwananchi mtandaoni 2022 na namini zitakusaidia
1: Uwe na tabia ya kupenda watu kwa moyo wote, hali kadhalika na wewe watakupenda.
2: Heshimu kila mtu na kila mtu umwone ni muhimu sana na wa maana.
3: Usimdharau mtu yeyote kutokana na hali yake,hata akiwa ni masikini ,hakuelimika,hana cheo cha juu na kadhalika.
4: Uwe mtu wa furaha na tabasamu unapokutana na watu.
5: Uwe mcheshi na mtu ambaye watu wanafurahi kuwa nawe.
6: Usipende kulaumu watu na kama utalaumu mtu,tumia njia nzuri na ya upole ya kumsaidia na kumjenga.
7: Usiwe msengenyaji na usimseme mtu vibaya.
8: Usipende kugombeza na kutukana au kutoa matusi kwa watu.
10: Usiwe mtu wa kujipendekeza kwa watu au wakubwa.
11: Usipende mabishano na kama yakitokea,usitake kila mara kushinda.
12: Uwe mpole na usiwe mkali kwa watu.
13: Usipende kugombana,kupiga au kupigana na watu.
14: Uwe mnyenyekevu na usijivune kwa kwa lolote lile,kama kuna jambo zuri kwako acha wengine wakusifu.
15: Usiwe na kinyongo,fitina na usitunze chuki.
16: Usilipize kisasi,badala yake tenda wema kwa Yule anayekukosea.
17: Usiwe unachonganisha watu,ukiambiwa udhaifu wa mtu usiende kumwambia aliyesema.
18: Jipende na kujikubali kama ulivyo kimaumbile na uwezo wako,ndipo na watu nao watakupenda na kukubali kama ulivyo.
19: Tunza siri zako na za wengine.
20: Usiwe mwepesi wa hasira
21: Kumbuka majina ya watu unaokutana nao.
22: Usiwe mzungumzaji kupita kiasi,badala yake uwe msikilizaji mzuri.
23: Usiseme uongo au kuongeza chumvi au kupotosha ukweli.
24: Zungumza kufuatana na mambo mtu anayoyapenda.
25: Maliza ugomvi au migogoro na wengine kwa njia ya amani kwa kuzungumza na mhusika.
26: Jifunze kusamehe makosa ya watu.
27: Unapofanya makosa, kubali na kuungama na kuomba msamaha.
28: Heshimu na kuvumilia mawazo na maoni ya wengine ambayo ni tofauti na yako. Asante