Mbinu mpya wanayotumia matapeli wanaotuma meseji

Mbinu mpya wanayotumia matapeli wanaotuma meseji

Zogoo da khama

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2013
Posts
631
Reaction score
592
Habarini za asubuhi,

Wale jamaa zetu wa "tuma kwenye namba hii" kisha wakaja na kauli mbiu yao ya "Mimi mwalimu mtoto wako ameanguka ghafla tunaomba utume pesa kidogo ya kusaidia matibabu ya haraka huku ukijiandaa kuja" wamekuja na kauli nyingine isemayo: "
Habari yako? Mimi mwenye nyumba wako naomba hiyo kodi ya nyumba irushie kwenye hii ttcl 0734 693 419 maana na shida nayo, halafu mbona umekaa kimnya bila taarifa?

Namba ya mtumaji 0734 457 719

Chukueni tahadhari wale mliopanga
 
Napokea meseji kama hii wakati naishi kwangu sijapanga, ila si ajabu kuna watu unakuta wanatuma hata kama wanakaa kwenye nyumba zao walizojenga wenyewe 😂 😅 watanzania hawana masihara
 
Leo nikiwa naelekea City Centre hapa Jijini Mwanza tukiwa daldalani ilipofika maeneo ya Kona ya Nyegezi kaingia bibi mmoja analia anadai katapeliwa laki nne na nusu kwenye simu na mtu aliyejitambulisha kama Padre wa Kanisa Katoliki Parokia ya Butimba.
Konda hakumdai nauli na dereva kamshusha Kanisani hapo ili "akapambane" na aliyemtapeli.
 
Mimi ninachojiuliza wanapataje hizi namba zetu maana dah! Aisee sielewi wanajuaje kuwa namba hii inatumika.

Au wanajuaje kwamba huyu mtu anapesa kwenye simu aana aisee.
 
Sasa hivi wamekuja na mbinu nyingine na hii nimeziona juzi. Jamaa yangu kapoteza simu juzi. Namjua muda mrefu tu kuwa anatumia simu ndogo. Sasa nimeshangaa napokea msg whatsapp kutoka kwenye namba yake nimuazime pesa kidogo. Nimesikitika Sana maana najua kuwa hata jamaa akienda kufunga line yake bado jamaa ataendelea kutapeli WhatsApp tu mpaka apate simu kubwa ya kutumia kufunga account yake
View attachment 1818372
 
TTCL wanazingua maana namba zao ndio zatumika kwenye hizo sms
 
mimi alinitumia ela 50000 halafu hapohapo akanipigia kwamba amekosea hivyo ananitumia namba ya dogo aliye skuli nimrushie...
nikampotezea maana janja ya nyani kwishajua!!
hadi mwisho ikaomba msamaha kwamba nirudishe haitarudia tena...
hapo mimi iko kwa mama muuza piga moja moto moja baridiiiii..
iko fikiri kila mtu ni MAKU MAKU
Hii nayo ikoje mkuu... yaani mfano ungefanya vile atakavyo ungeibiwaje?
 
mimi alinitumia ela 50000 halafu hapohapo akanipigia kwamba amekosea hivyo ananitumia namba ya dogo aliye skuli nimrushie...
nikampotezea maana janja ya nyani kwishajua!!
hadi mwisho ikaomba msamaha kwamba nirudishe haitarudia tena...
hapo mimi iko kwa mama muuza piga moja moto moja baridiiiii..
iko fikiri kila mtu ni MAKU MAKU
yaani sijaelewa alituma hiyo hela ili iweje Bado nipo gizani mkuu!
😂😂😂😂
 
Leo nikiwa naelekea City Centre hapa Jijini Mwanza tukiwa daldalani ilipofika maeneo ya Kona ya Nyegezi kaingia bibi mmoja analia anadai katapeliwa laki nne na nusu kwenye simu na mtu aliyejitambulisha kama Padre wa Kanisa Katoliki Parokia ya Butimba.
Konda hakumdai nauli na dereva kamshusha Kanisani hapo ili "akapambane" na aliyemtapeli.
daaa matapeli hawana adabu bwasheee
😂😂😂😂
 
Napokea meseji kama hii wakati naishi kwangu sijapanga, ila si ajabu kuna watu unakuta wanatuma hata kama wanakaa kwenye nyumba zao walizojenga wenyewe 😂 😅 watanzania hawana masihara
Au unatumiwa hiyo msg wakati Baba Mwenyenyumba umemlipa jana tu.
 
Leo nikiwa naelekea City Centre hapa Jijini Mwanza tukiwa daldalani ilipofika maeneo ya Kona ya Nyegezi kaingia bibi mmoja analia anadai katapeliwa laki nne na nusu kwenye simu na mtu aliyejitambulisha kama Padre wa Kanisa Katoliki Parokia ya Butimba.
Konda hakumdai nauli na dereva kamshusha Kanisani hapo ili "akapambane" na aliyemtapeli.
Huyo bibi anaweza kuwa ndio kamtapeli konda nauli yake kwa kisigizio hicho
 
Sms hiyo ilinikosa kosa mwaka jana... ilikuwa hivi;

Nimeongea na mama mwenye nyumba kama leo akanambia kuwa hela ya nyumba tuangalie tu chochote cha kufanya (marekebisho kwenye nyumba yake hasa chooni).

Siku mbili mbele huwezi amini iliingia sms hivyohivyo ulivyoandika basi nikakasirika nikaanza kuipigia ile namba iliyotuma sms. Kila nikipiga mara ya mwanzo bize mara ikawa inakatwa mara simu hairuki

Sasa yule mama kibaya zaidi ni mtu bize (yupo Dar ana biashara zake) kwahiyo mara nyingi ili umpate au ili aweze kupokea simu ni jioni kuanzia saa moja basi nikipiga ile namba yake ya siku zote nikawa simpati.

Mola tu... nikasema ngoja nimsikilizie kwanza huku najiuliza kwanini amenichenjia hivi hadi namba katumia airtel nyingine (kipindi hiko ndo naanza kuziona namba za 069... halafu yakwake halisi na hiyo ilotuma sms zilikuwa zafanana)

Basi kesho yake nikampigia namuuliza una airtel ngapi maana nimeona ujumbe wako jana aisee alishangaa na ndipo akanifungua macho kwa kusema "hao ni matapeli usibabaike nao, mimi haitakaa nichukue hela yenu huko kijijini- cha msingi mnitunzie nyumba yangu".

Basi na kweli mpaka nimehama pale yule mwenye nyumba kuonana nae ni mara moja tu (wala sidhani kama namkumbuka vizuri sura) na sijawahi kulipa hela ya kodi zaidi ya kufanya matengenezo ya marekebisho tu ya pale pale
 
Habarini za asubuhi,

Wale jamaa zetu wa "tuma kwenye namba hii" kisha wakaja na kauli mbiu yao ya "Mimi mwalimu mtoto wako ameanguka ghafla tunaomba utume pesa kidogo ya kusaidia matibabu ya haraka huku ukijiandaa kuja" wamekuja na kauli nyingine isemayo: "
Habari yako? Mimi mwenye nyumba wako naomba hiyo kodi ya nyumba irushie kwenye hii ttcl 0734 693 419 maana na shida nayo, halafu mbona umekaa kimnya bila taarifa?

Namba ya mtumaji 0734 457 719

Chukueni tahadhari wale mliopanga
Naona kuna loophole Kwa Tccl number zao zinatumiwa Sana na hawa matepeli, alafu hata ukiripoti hizo namba TCRA naona hakuna hatua, kuna mmoja amewahi kunitumia nitakafoward ujumbe TCRA, lakini baada ya mwezi namba Ile Ile tena ikatuma ujumbe kuwa Mtoto anaumwa shule
 
yaani sijaelewa alituma hiyo hela ili iweje Bado nipo gizani mkuu!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Itakuwa alitumiwa msg ya pesa, lakini sio pesa. Matapeli waga wabahili kweli. Ukimwambia kwa kuwa nimeshinda sh milioni tano, we tumia gharama zako za ku proccess ushindi hela ikitoka nitakulipa na faida huwa hawakubali. [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Habarini za asubuhi,

Wale jamaa zetu wa "tuma kwenye namba hii" kisha wakaja na kauli mbiu yao ya "Mimi mwalimu mtoto wako ameanguka ghafla tunaomba utume pesa kidogo ya kusaidia matibabu ya haraka huku ukijiandaa kuja" wamekuja na kauli nyingine isemayo: "
Habari yako? Mimi mwenye nyumba wako naomba hiyo kodi ya nyumba irushie kwenye hii ttcl 0734 693 419 maana na shida nayo, halafu mbona umekaa kimnya bila taarifa?

Namba ya mtumaji 0734 457 719

Chukueni tahadhari wale mliopanga
Zote hizo kwa pamoja zipo kwa muda mrefu sana, ni upumbavu kwa mtu kuweza kufanya muamala wa fedha kwenda namba usiyoijua na bila kuwasiliana na huyo unayedhani ndio unamtumia kwenye namba unayoijua

Atleast pale ambapo mtu unayemjua ameibiwa simu halafu ndio ikatumika namba ileile unayoijua kukutumia ujumbe
 
Hili suala ni kweli, wazazi wangu walitaka kutapeliwa kwa mtindo huo, nina mdogo wangu kamaliza 4m 6 mwaka huu, sasa wakati yuko shule ilikua mwezi wa pili,

Siku hiyo majira ya mchana baba akiwa kazini kwake, akapokea sms kwa cm yake ikisomeka hivi, "habari mzazi, mwanao ameanguka darasani ghafla na kupoteza fahamu, tumefanya jitihada za haraka kumfikisha hospital ambapo anapatiwa matibabu, ila bado hajapata fahamu hivyo unatakiwa utume gharama za matibabu kwa no hii (huku ikiambatanishwa namba husika)".

Baada ya kusoma ile sms, akahamaki akampigia cm mama kumfahamisha, hapo mama akaanza kuchanganyikiwa na kumshinikiza baba atume hela haraka iwezekanavyo, sasa baba akatak kujua undani wa tukio hilo, akapiga cm kwa no ilotuma text haipokelew zaid ya mara 3, baadae ile no ilatuma sms "samahani nipo sehemu mbaya siwezi kupokea cm, ila mwanao kazinduka na daktari kasema gharama itakua laki 2".

Hapo baba akaona haelewi chochote, akamtafuta kaka mkubwa kumpa taarifa, sasa mkubwa ana mawasiliano na baadhi ya walimu ktk shule anayosoma dogo, akawacheki kuuliza anambiwa dogo yupo vizur wala hakna tatzo lolote, akapewa dogo cm wakaongea na kaka yaan dogo yupo vizuri kabisa. Ndo hapo ikawa amani kwa wazazi, vinginevyo wangetuma hela kwa matapeli.

Utapeli wa mtandaoni upo na unazidi kukua kwa kasi.
 
Itakuwa alitumiwa msg ya pesa, lakini sio pesa. Matapeli waga wabahili kweli. Ukimwambia kwa kuwa nimeshinda sh milioni tano, we tumia gharama zako za ku proccess ushindi hela ikitoka nitakulipa na faida huwa hawakubali. [emoji16][emoji16][emoji16]
Matapeli wanatuma msg ya muamala tu na sio pesa, afu anakwambia nimekosea naomba unirudishie
 
Back
Top Bottom