Amba Samedi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2024
- 207
- 346
WanaJF habari za leo,
Ni saa 2:11 kamili hapa Morogoro niliko. Sasa leo hali ya hewa imeamua kuja kiaina: ukungu wa kutosha, kabaridi kwa mbali. Na bado nkaondoka nyumbani saa 11 kujiandaa kwa kazi na kukuandikia maneno haya.
Jana katika pitapita zangu nimekutana na mbinu moja ya kishujaa kweli. Siku zote huwa napata shida sana kusaka wateja (hasa local clients) wa humu nchini, kwa ajili ya kuendeleza biashara yangu. Sasa, nilipata mbinu nzuri mno ambayo ntashare na wewe sasa. Kaa mkao wa kula maarifa.
Google Maps ni Nini?
Kwa wageni, Google Maps ni mfumo wa ramani iliyotengenezwa na kampuni ya Google. Ukiwa na biashara na ukafanikiwa kuiweka kwenye ramani ya Google, inakuwa rahisi sana kwa wateja kukupata, ama kwa njia ya kusaka usafiri kutumia apps kama Uber na Taxify, au via simple Google search.
Endapo ushasoma mpaka hapa na biashara yako haipo hewani, unakosa wateja. Endapo utahitaji msaada wa kupandisha, nivutie waya ntakusaidia/kukuelekeza, bure kabisa.
Kutafuta Wateja Kutumia Google Maps
Sasa ni muda wa kupata wateja. Kwa mfano, unataka kussuply nyama kwa wauza butcher Dar-es-salaam. Fanya yafuatayo:
1. Fungua Google Maps. Nenda Google Maps ili kufikia page ya maps.
2. Ingiza maneno haya "Butchers in Dar-es-salaam" kwenye search bar kama nlivyofanya hapo chini, kisha bofya "Search" ili kugenerate list.
Utaona page kama hiyo hapo ilojitokeza. Ina list ya butcher zilizopandishwa tayari (kwa maoni yangu ni chache mno. Wafanyabiashara tufanye mpango kuwa na online presence).
Hapo kwenye Results, unaweza kuscroll ili kuona orodha za butcher zote zilizokuwa listed. Ukiclick mojawapo, utaona details za biashara.
Kwenye mfano uliopo hapo chini, nimeclick Dresa Modern Butcher, na details zake zinaonekana hapo, ikiwemo namba ya simu ambayo naweza kutumia kuwasiliana na mwenye bucha na kummuzia idea yangu:
Kwa haraka haraka, hizo listing ni zaidi ya 100. Kuanza kucopy details moja moja utachukua muda kidogo. Ili kwenda haraka, ntakuonyesha sasa mbinu moja rahisi ya kupata contacts zote hizo ndani ya dakika 5.
Mbinu"Otomatiki" Ya Kupakua Leads (Orodha ya Wateja ) Wengi Kwa Mpigo
Asante kwa kuendelea kufuatilia. Ili kuendelea, fanya hivi:
1. Pakua Chrome Extension yenye jina Easy Scraper. Type neno "Easy Scraper Chrome Extension" kwenye Google, kisha press enter.
Inafanana hivi:
Bofya hiyo button ya Add to Chrome ili kuiongezea kwenye Chrome. Unaweza kuipin ili iwe rahisi kuitimua. Inafanana hivi (baada ya kuinstall):
2. Nenda kwenye page ambayo tulifungua yenye list ya biashara za bucha. Kisha fungua Easy scraper. Utaona screen kama hii hapa:
Utagundua kuwa ishakutengenezea orodha ya biashara ambazo zimekuwa listed. Ili kupata biashara zote, nenda kwenye drop down yenye jina Action to load more items, kisha chagua menu inayosema Scroll down to load more items.
Bofya Start Scraping ili kugenerate list ya biashara zote zilizopo kwenye page. App ya Scraper itascroll list nzima na kufanya hivyo kwa niaba yako.
Matokeo! Nina list ya biashara 120, niliyotengeneza ndani ya sekunde 22 kutumia hii app. Ukitaka, unaweza kumaximize screen ili kusafisha list ilopewa na kubaki na data unazohitaji. Mimi nlitaka jina la biashara, location, aina, delivery type, rating na namba ya simu. Baada ya kusafisha, nkabaki na data ifuatayo:
Bonus: Unaweza kubadilisha titles za pale juu ili kureflect unachotaka, kama nlivyofanya. Bofya CSV ili kupata data kwa njia ya CSV ambayo unaweza kutumia kwenye apps kama Excel kwa ajili ya kuwapigia simu na kunote walichosema.
Kwa wale mnaopenda ChatGPT, unaweza kuiweka humo ili ikusaidie kubadilisha baadhi ya vitu, kama kuongeza column, kutunga ujumbe kwa ajili ya mteja, nk.
Hitimisho
Nimekupa mbinu mojawapo ya kujipatia "local clients" kwa kutumia google maps. Inshallah, ntaleta mbinu zingine in the coming future (ikiwemo ya Instagram, Facebook Groups na Google Search). Na mbinu hizi hazina gharama yoyote. Ni wewe, muda na ujuzi wa kutumia tools hizi.
Je, una ujanja mwingine kama huu? Au kuna kitu hakijaeleweka? Share na sisi!