Tomaa Mireni
JF-Expert Member
- Sep 8, 2015
- 2,395
- 2,391
Hivi karibuni tumeshuhudia nchi mbalimbali ziiathirika na majanga ya mafuriko na mioto ya msituni. Je ushajiuliza kama janga kama hilo likitokea eno lako hatua za kuchukua na hatua gani ya kuanza nayo?
Nchi ambazo zina miundombinu bora lakini bado zimeathiriwa na mafuriko kama Ujerumani, Ubelgiji, Uturuki na ulaya karibu yote, China na India pia. Vipi kwa Tanzania ambao wakazi wengi wanajenga mabondeni na kutokufuata ushauri wa ujenzi bora? Bila shaka huenda kukawa na maafa zaidi.
Hapa nitatoa mbinu iwapo kutatokea janga la mafuriko sababu ndio lina nafasi kubwa kuliko mioto ya msituni na matetemeko,japo baadhi ya mbinu zinaingiliana pia.
MAANDALIZI YA MUDA MREFU
Pole nyingi ziende kwa nchi ya Haiti kwa kupoteza raia wao kwa tetemeko la ardhi lenye uharibifu mkubwa sana.
Ruksa kujazia nilivyosahau.

- Kama unaishi maeneo ya mabondeni unaweza kujiwekea lengo la kununua kiwanja sehemu iliyopimwa na kujenga taratibu.
- Unaweza kusafisha mitaro inayopita karibu na makazi yako ili yasizuie maji pindi mvua inaponyesha kwa wingi.
- Unaweza kuzibua mitaro iliyoziba kwa matakataka ili maji yapite kiurahisi yasilete madhara nyumbani kwako.
- Cha kwanza kabisa ni kuwa mfuatiliaji wa habari za hali ya hewa mbalimbali iwe ni kwenye radio, televisheni au hata kwenye mitandao ya kijamii.
- Tii serikali inapotoa muongozo bila kupuuza na kujipa moyo kuwa ngoja usikilizie kwanza kama kuna madhara.
- Tenga kila mtu na mkoba/begi lake ambalo kama ikitolewa tahadhari mnaweza kubeba kirahisi. Begi hilo linapaswa kuwa na vitu muhimu kama. Kadi ya benki, fedha kidogo,maji ya kunywa,dawa,shuka 1 na nguo nzito.
- Ukiona dalili ya maji kuwa mengi eneo lako toka nenda sehemu salama,iliyotengwa na serikali au maeneo yaliyoinuka.
- Usihangakie kuokoa vitu vingine vya ndani kwani ni hatari unaweza kupoteza uhai wako ambao hauwezi kununua popote.
Pole nyingi ziende kwa nchi ya Haiti kwa kupoteza raia wao kwa tetemeko la ardhi lenye uharibifu mkubwa sana.
Ruksa kujazia nilivyosahau.