Christopher Chege Msando hakuwa mfuasi wa chama chochote kile na alitaka ku-introduce huo mfumo mpya wa kielektroniki kuwafanya wakenya wapate taswira halisi ya matokeo ya uchaguzi.
Msando akiwa ni mtaalam na pioneer mkubwa wa masuala ya teknolojia, alitaka kutumia utaalam wake kujaribu mfumo mpya wa upigaji kura kielektroniki.
Alikuwa na taarifa zote za ndani ya mfumo huo yaani passwords, IS au information system ambayo ingetumika kutuma matokeo na kuyahifadhi mtandaoni.
Pia alikuwa na jukumu la kutunza taarifa za wapiga kura, kama majina, namba za kujiandikisha, na namna mfumo huo ungeweza kuoanisha matokeo ya upigaji kura tarehe 8 August.
Hivyo kwa ushawishi wa NASA na Jubelee (kwa shingo upande) akafanikiwa kuuboresha mfumo huo na kuuwezesha kuwa wa kisasa zaidi kuwahi kutokea Afrika Mashariki.
Hivyo alipenda awaonyeshe wakenya utaalam wake huo tarehe 1 August jinsi unavyofanya kazi na manufaa yake.
Hivyo kwanza ni Msando ni mtu asiye na chama halafu anaunda mfumo wa kompyuta wa upigaji kura nchi nzima ili kudhibiti upigiaji kura uwe wa haki.
Pili, alitaka awape elimu wapiga kura kuhusu mfumo huo.
Ukifanya hivyo kwenye nchi kama Kenya ambayo asilimia kubwa na uchumi wake unawategemea walowezi wa kutoka Uingereza na wakenya wachache ambao ndiyo wanaoiendesha nchi hiyo, basi unakuwa unawakwaza sana watu hawa.
Kwasababu ni lazima garimoshi iendeleee kusonga mbele kwa ule mlio wa "kata mti, kata mti, kata mti......"
Unakuwa kikwazo kwa maendeleo, yaani "obstacle to progress"