jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 36,197
- 29,717
Tunaposheherekea miaka 63 ya Uhuru ni vyema kama Taifa kutafakari katika maeneo kadhaa ambayo ni muhimu.
1-Tanganyika ilipata uhuru bila kumwaga damu yaani vita.
2-Kupitia Waasisi wetu hususani Mwalimu Nyerere tuliona njia bora ni kudai Uhuru wetu kwa njia ya kidiplomasia.
3-Hata baada ya kupata Uhuru bado tuliamini diplomasia ni njia bora ya kuendelea kuulinda Uhuru.
Hatukujielekeza katika kisasi dhidi ya wakoloni ama vibaraka wake.
4-Tulitambua udhaifu wetu kiuchumi na tuliheshimu sana Maguvu waliyonayo wakoloni.
5-Waasisi wetu hawakuwa wabinafsi kwani kuna baadhi ya mengi ambayo yangeweza kuleta maendeleo kwa haraka waliyaacha kama mikakati wakisubiri kizazi kijacho kuja kufanyia kazi kwa muktadha ule ule wa uvumilivu na subra.
6-Vita vya kagera viliturudisha nyuma kiuchumi na kihuduma lakini ilikuwa muhimu kwa kipindi hicho kupeleka ujumbe kwa majirani zetu na vibaraka wote wa wakoloni.
7-Tumetumia mbinu nyingi sana za mafanikio katika kukwepa majanga yatokanayo na proxy wars za wababe wawili wa kidunia.
mbinu hii imetuvusha hadi sasa na kutufanya tuendelee.
8-Imekuwepo na itaendelea kuwepo nia ovu ya wababe wa dunia kutaka tuingie kwenye mchafuko mwingine ili tu iwe rahisi kuchota rasilimali zetu kwa manufaa yao.
9-Bado upo mshangao mkubwa duniani wa mataifa katili yenye kuhodhi njia za uchumi duniani kuona kwa nini tuna amani hadi sasa...kumbuka amani ni msingi wa uchumi imara na taifa tishio kwa siku zijazo.
10-Upo sasa mkakati rasmi wa kuifanya Tanzania iwe unstable isitawalike au iingie kwenye machafuko.
11-Vijana wasomi ambao ni matokeo ya sera bora na mikakati mizuri wameongezeka na bado hatujaweza kuwa-accomodate katika sekta zitakazo wapa fursa.
12-Kama Taifa sasa inabidi kuja na sera mpya na mahsusi kwa vijana ambao wameelimika.
13-Ipo haja sasa ya kurejea mikakati tuliyowahi kuitekeleza hapo awali mfano sekta ya michezo na utamaduni,Sekta ya viwanda ,ujamaa na kujitegemea n.k ambapo itavyonza kundi hili kubwa linaloongezeka mtaani.
14-Kama Taifa pia inatupasa kuset standard ya nani anapaswa kuthaminiwa inapokuja swala la mafanikio mfano...tuwatambue vijana wenye uwezo wa kiakili shuleni,wenye uwezo katika michezo,wenye uwezo wa biashara,wenye uwezo wa sayansi n.k
Tuondokane na kasumba ya kuthamini wenye mafanikio yasioeleweka yamepatikana vipi.
Tufute role models mithili ya mwijako,babalevi na comedians wengine.
Naamini Profesa Palamagamba Kabudi anafaa kuhuisha uzalendo kwa vijana kupitia utamaduni(a strategic choice)
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!! TISA DISEMBA!!