Nami naunga mkono yote yalitajwa na wenzangu hapo juu,ila ningependa niongeze yafuatayo;
1.Tafuta Madesa/simbi za kutosha za kila soma,zipitie vizuri,uzielewe vizuri kabisa na na hata ishindikana waweza kubeba/kukariri,na ili uzielewe vizuri zipitie kwanza wewe mwenyewe baada ya kutoka pindi then nenda kwenye group discussion.Huko kwenye discussion shiriki kikamilifu....Madesa/Simbi zitakupa mwanga Lecturer huwa anakuja kinamna gani,pia hao malectures wengi wao siku hizi hawana muda na mambo ya shule kwa sana,wengi wao wana viNGOs or Washauri kwenye makampuni/mashirika ambako hulipwa fedha nyingi ,hivyo ikifika kipindi cha mitihani huwa wanachukua past papers na kuzidurufu kama zilivyo,wengine husahau hata kubadilisha mwaka
2.Mwisho kuwa makini kwenye uchaguzi wa marafiki,angalia wale wenye tabia nzuri na vipanga,watakusaidia sana
Kila la kheri kijana...Simbi zidumu!