Mbinu za CCM tu ndizo zitakazomuwezesha Mangungu na genge lake kushinda tena nafasi za uongozi Simba

Mbinu za CCM tu ndizo zitakazomuwezesha Mangungu na genge lake kushinda tena nafasi za uongozi Simba

NgerukeAbra

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2022
Posts
4,253
Reaction score
5,789
Kwa mujibu wa katiba ya Simba viongozi wote wa kuchaguliwa wanafika ukomo mwezi huu mwishoni.

Hadi sasa wanasimba hatuoni dalili yoyote ya uchaguzi tukimaanisha hakuna kamati iliyotangazwa kwa mujibu wa katiba kuendesha zoezi hilo kuanzia hatua za awali ambazo ni kutangazwa tarehe ya uchaguzi, zoezi la kuchukua fomu na kuzirudisha, usaili pamoja na mchujo kwa nafasi husika.

Mangungu kwenye mkutano uliopita aliahidi kuwa wanachama wapya wataanza kusajiliwa kuanzia tarehe 05/01/2026 cha ajabu hadi leo hii zoezi hilo halijaanza na hakuna tamko lolote toka kwa Mwenyekiti.

Watu wa karibu na Mangungu mwambieni atumie mbinu za CCM ili yeye na viongozi wenzake warudi tena madarakani.

1. Ateue wajumbe wote wa kamati ya uchaguzi.

2.Washindani wake wa kweli ahakikishe wanapelekwa polisi na kufungulia kesi za mchongo.

3.Aandae washindani feki wengi ili kuiaminisha jamii kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki

4.Kamati ikishamtangaza kuwa mshindi hakuna mamlaka yoyote inayoweza kuhoji au kupinga ushindi.

5.Uchaguzi uanze jioni giza likishaingia umeme ukatwe ukumbini na Mangungu atangazwe mshindi haraka sana.
 
Mangungu kamaliza muda wake hawezi kugombea tena labda atumie mbinu ya Karia ila amechelewa angeingiza kipengele kwenye mkutano mkuu uliopita.
 
Shida sio Mangungu.
Maamuzi yote yanafanywa na bodi ya wadhamini.

Mwenyekiti hana kura turufu.
Akiingia kwenye kikao cha wadhamini yeye anakuwa sawa na kila mjumbe kwenye suala la kuamua nn kifanyike.

Bodi ya wadhamini ina watu 9 kutoka kwa wadhamini ambao wanachaguliwa na mwekezaji.

Na ina watu 6 ambao wanachaguliwa na wanachama.

Kwahiyo ni 9 vs 6.

Shida inaanzia hapa. Katiba inampa nguvu mdhamini kuliko mwenyekiti aliyechaguliwa na wanachama.
 
Back
Top Bottom