Mbinu za kimasoko (Marketing tactics)

Hii imekaa poa sana mkuu, sema mawazo ya biashara pia ni changamoto..? hili unalionaje mkuu
 
Asante kwa somo zuri, mimi ninahitaji msaada wako katika biashara ambayo imeanguka kisha ina madeni mengi na kwa sasa ninajipanga kuifufua upya. Kwa kifupi ni kwamba nilikuwa naendesha biashara ya bakery kwa kipindi cha miaka 6, lakini kwa bahati mbaya mwaka 2016 nilivunjiwa mahali nilipokuwa nafanyia biashara hii, kitendo hicho kiliniingiza kwenye matatizo makubwa sana kwani nilikuwa na mikopo mikubwa kwenye mabenki na kwa washirika wa biashara ambao walikuwa wananipatia malighafi na wengine vitendea kazi. Baada ya kuvunjiwa nimekaa miaka 2 ninahangaika kuona kama ninaweza kurudi tena kwenye game bila mafanikio kutokana na ukubwa wa madeni niliyokuwa nayo, mpaka nikaanza kuuza baadhi ya asset ili niweze kuanza tena lakini nilishindwa kwani madeni yalikuwa mengi. Kwa sasa nimeanza tena lakini biashara ni changa na matumizi ni makubwa kuliko kipato hivyo inanipata changamoto ya namna ya kujiendesha. Wewe kama mtaalamu unanishauri nifanye nini ili biashara iweze kusimama tena?
 
Ngoja nikwambie kitu.

Kwenye biashara ni vitu viwili tu ndiyo vinavyoweza kukuletea faida.

1. Innovation

2. Marketing

Mambo mengine yote ni Cost tu.

Nimejifunza haya kupitia uzoefu.

Nikiongelea kwaufupi kuhusu Innovation ni kwamba kama unaendelea kufanya biashara yako bila kuwa mbunifu soon you will be out of business. Ubunifu ni mambo yote kuanzia unavyoandaa mikate yako, utamu wake, ingredients unatumia.....everything.

Pia niongee Marketing kidogo.

Watu wengi wanadhani marketing ni kuandaa tangazo na ku-post sehemu basi tayari umemaliza. No way this is going to work.

Lazima uwe na Marketing strategy. And marketing strategy unaweza kuitengeneza kwakuwaelewa wateja wako. Don't lie to yourself you are smart than your customers. Tafuta njia yakufahamu nini wanataka hasa. Na namna gani wanapenda wahudumiwe. Utajifunza mengi.

Mwisho niseme, jaribu kupunguza gharama kwakuweka msisitizo kwenye Innovation na Marketing.
 
Umemshauri vizuri sana Mkuu.
Ahsante.
 
Mkuu, unapatikana wapi?
Waweza nitafuta kwa namba yangu hapo juu kwa mawasiliano zaidi.
Karibu Sana.
 
Somo zuri but nina ushauri binafsi.......

Ni kwamba katika ulimwengu wa masoko, "drive" ya mafanikio ni flexibility..... Hivyo basi techniques kama hizi ambazo zimekuwapo for decades huwa zinakuwa ni useless after a period of time....

Ni sawa sawa na vitani, hauwezi shambulia adui na silaha ya zamani katika vita/ugomvi mpya! Tafasiri yake ni kuwa unampa adui nafasi ya kujua madhaifu ya silaha yako na kujikinga nayo na pia kutengeneza imara zaidi.....

So free advise ni katika masoko/marketing profession........Hakuna kitu kibaya kama kuklemisha njia za mafanikio ama sivyo itakugharimu, muda, na pesa........

Kimsingi marketing inataka active brain yenye open eyes to details......

Most companies wanafeli kwa kuajiri wasomi waliograduate kwa kumeza makitu au vitu ambavyo currently vina impact ndogo ama hakuna kabisa impact.....!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…