Mbinu za kubana matumizi ya mafuta kwenye gari yako

muzi

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2016
Posts
1,041
Reaction score
1,457
Dar es Salaam. Wako wanaofikiria kupumzisha magari yao kutokana na mzigo mkubwa wa gharama za kuyatumia, na hasa bei ya mafuta ambayo inaendelea kupanda, huku kipato kikiendelea kudumaa.

Baadhi wanaweza kuingia katika majaribu ya kununua petroli kwa bei rahisi mitaani wakati ubora wake umeshapunguzwa baada ya wauzaji kuichakachua kwa kuichanganya na mafuta ya taa na hivyo kuwa hatari kwa injini.

Wakati hali ya kiuchumi ikizidi kuwa ngumu kwa Watanzania wengi, ambao wanaona mkakati wa Serikali wa kubana matumizi umewaathiri, gazeti la Mwananchi linalo suluhisho la kukuwezesha uendelee kutumia gari lako katika mazingira hayo.

Wataalamu waliozungumza na mwandishi wetu wameeleza mbinu kadhaa za kumuwezesha mtumiaji gari kuepuka kutumia mafuta mengi wakati anapoliendesha na hivyo kujipunguzia mzigo wa gharama za mafuta.

Mbinu hizo zinahusisha kutembea wakati hakuna foleni; kwa safari ndefu, kutumia kiyoyozi; madereva kubadili hulka zao, matunzo na muundo wa gari na ubebaji wa mizigo mizito.
 
Kuna utaratibu wa kusaidia gari isitumie zaid mafuta kwanza kabisa ni service on time ya engine oils na kila kitu,nozel kufanya kaz vzr,kuna kitu kinaitwa air filter kazi yake kuchuja hewa inayoingia kwenye mfumo wa injini so ikiwa chafu hii air filter inasababisha injini kupokea hewa chafu na kutumia nguvu nyingi wakari ukiendesha na kupelekea ulaji wa mafuta,kuna cable zikiwa mbov au moja wapo ikiwa inachoma nje inasababisha gari kumis so inapelekea mafuta mengne kutolipuliwa vzr yaan kua mabich na kupelekea mis
 
ni bora wewe kuliko mtoa mada
 
ni bora wewe kuliko mtoa mada
Pia kuna sababu nyingne kama urembo,unapoongeza size ya rim au kufunga tairi kubwa zaidi pia inaongeza ulaji kwa sababu unakua umeongeza mzunguko wa tairi,
maxresdefault-5707fc96ddf9b.jpg
 
Kuna utaratibu wa kusaidia gari isitumie zaid mafuta kwanza kabisa ni service on time ya engine oils na kila kitu,nozel kufanya kaz vzr,kuna kitu kinaitwa air filter kazi yake kuchuja hewa inayoingia kwenye mfumo wa injini so ikiwa chafu hii air filter inasababisha injini kupokea hewa chafu na kutumia nguvu nyingi wakari ukiendesha na kupelekea ulaji wa mafuta,kuna cable zikiwa mbov au moja wapo ikiwa inachoma nje inasababisha gari kumis so inapelekea mafuta mengne kutolipuliwa vzr yaan kua mabich na kupelekea mis

Yeah hii ni kweli kabisa, lakini pia sababu zingine zinazochangia ulaji wa mafuta. Zaidi ya hayo pia kuna swala la kutumia gia ya ya kuendeshea especially kwenye hay magari ya manual pia automatic somewhere. Unakuta njia tambarare gari inahitaji gia namba 5 au 6 lakini mtu unaebdeshea namba 3. Kwenye automatic ni pale ambapo unataka kukimbia speed zaidi unaweka ON kitufe cha OVERDRIVE. Hapo kwa kweli utavutika speedy sana lakini mafuta utaisoma namba. Kinachotokea ni kwamba kama gari ilikuwa namba 4, ukiweka kitufe ON gia ya automatic inarudi namba 3 na kuongeza acceleration na momentum kwa kasi zaidi. Pia basipo kufanya service on time nayo pia huchangia kwa kiasi kikubwa kama ilvyoelezwa hapo juu
 
Yah mkuu pia kuna inshu ya plugs pia kama zimechoka,chafu,fake nazo zinachangakia kwa sababu wakati wa ulipuaji inatokea miss fire,hazichomi vizuri
 
Yeah hii ni kweli kabisa, lakini pia sababu zingine zinazochangia ulaji wa mafuta. Zaidi ya hayo pia kuna swala la kutumia gia ya ya kuendeshea especially kwenye hay magari ya manual pia automatic somewhere. Unakuta njia tambarare gari inahitaji gia namba 5 au 6 lakini mtu unaebdeshea namba 3. Kwenye automatic ni pale ambapo unataka kukimbia speed zaidi unaweka ON kitufe cha OVERDRIVE. Hapo kwa kweli utavutika speedy sana lakini mafuta utaisoma namba. Kinachotokea ni kwamba kama gari ilikuwa namba 4, ukiweka kitufe ON gia ya automatic inarudi namba 3 na kuongeza acceleration na momentum kwa kasi zaidi. Pia basipo kufanya service on time nayo pia huchangia kwa kiasi kikubwa kama ilvyoelezwa hapo juu
Yaani gari inatoka gia na 4 kurudi 3 halafu unasema spidi inaongezeka!!!??? Sayansi ya wapi hii??
Kiuhalisia unapofanya hivyo unaifanya gari kuwa na nguvu zaidi kwa kuwa itakuwa inatembelea gia kubwa lakini mwendo unapungua.
 
Sijaelewa kidogo kwani katika automatic gear kuna gear ngapi .
Just for my normal understanding ukiweka D unaruhusu Gari kutembea hadi gear ya 3 but ukiweka d2 unaruhusu gar kutembea hadi gear ya 2 yani 2nd gear.
Na ukiweka L unaruhusu Gari kutembea na gear ya chini kabisa ambayo ni 1 ..
Kwamfano nikiweka overdrive nikiwa L Gari litaongeza kasi au lita maintain steady speed?
 
Back
Top Bottom