Geofree, kufaulu hesabu ni rahisi ikiwa utazingatia yafuatayo:
1.
Ipende hesabu, achana na lugha za mitaani za wasiojiweza na wasiojielewa kama vile"HESABU UGONJWA WA KITAIFA", wengine "JANGA LA TAIFA" nk.
2. Fanya mazoez mengi, hii itakusaidia kupata uzoefu wa aina tofautitofauti za maswali, na pia utaboresha spidi ya kusolve hesabu kwa wakati. SPIDI hapa ni factor ya muhimu sana katika kufaulu hili somo. Kuwa na mazoea ya kusoma hesabu kila siku iendayo kwa Mungu, hata ukitenda dk 30 kila siku ukazitumia vizuri zinatosha kabisa.
3. Usikate tamaa, ukishindwa swali, muulize mwenzako, ikishindikana kabisa miongoni mwa wanafunzi wenzako, muone mwalimu akusaidie. Lakini pia, ukishindwa leo, jaribu kesho, keshokutwa nk. Hii njia itakusaidia, na hakuna kitakachokushnda.
4.hakikisha kabla ya kufanya mtihani wako wa taifa, Mock nk, uwe umefahamu mada nyingi kuanzia form 1 hadi 4. Usidharau topics ambazo huwa na maswali madogo madogo kwenye mitihani na kuwa na uzito wa maksi 3 hadi 6, hizo ndizo zitakusaidia kufikisha maksi nyingi. Wanasema "KIDOGO KIDOGO HUJAZA KIBABA". Kaa ukijua wanaotunga mtihani wa taifa hawajali kama umekamilisha mada au lah! Wale hawajua tabu watu wanazopata ktk shule za kata, kama vile kusoma topics 2 tu kwa mwaka mzima nk.
5. Kama wewe unaona haujafanya maandalizi ya kutosha, na hauna muda (mf. Form 4 kwa sasa wana takriban miezi 2), embu komaa na mada chache ambazo ni rahisi kwako kuelewa na utazipenda. Mf. Statistics, hii topic ipo kwenye hesabu na geograph, na hutoka section B (10 marks) hivyo ukiielewa vzuri utafaidika mara 2. Hapa ongeza na topics nyingine 2 au 3 ambazo hutoka section B, na unaweza kujiokoa na F. Unaweza kutafuta mtu wa kukusaidia ktk topics ulizochagua.