Mbinu za kufaulu somo la Hesabu (O-Level)

Geofree

Member
Joined
Aug 18, 2014
Posts
44
Reaction score
5
Ninahitaji kujua mbinu za kufaulu somo la hesabu(MATHEMATICS) ukiwa O-LEVEL..

Topic zipi hasa zakutilia mkazo ili kufaulu
 
function,statitists,account, linear programing, and matrix and transformation. utatoka
 
topic zote ni muhimu kuzijua huwezi soma topic moja ikakutoa
 
Ninachokumbuka kiufupi pindi niko St kayumba A ya B/math niliipata kwa kusoma topics zote kwa wakati, kufanya maswali mengi per day( angalau 20 qns) na kufanya test za B/math kila wiki hasa ufikapo f4 na kumuomba Mungu kabla ya yote.
 
Geofree, kufaulu hesabu ni rahisi ikiwa utazingatia yafuatayo:
1. Ipende hesabu, achana na lugha za mitaani za wasiojiweza na wasiojielewa kama vile"HESABU UGONJWA WA KITAIFA", wengine "JANGA LA TAIFA" nk.

2. Fanya mazoez mengi, hii itakusaidia kupata uzoefu wa aina tofautitofauti za maswali, na pia utaboresha spidi ya kusolve hesabu kwa wakati. SPIDI hapa ni factor ya muhimu sana katika kufaulu hili somo. Kuwa na mazoea ya kusoma hesabu kila siku iendayo kwa Mungu, hata ukitenda dk 30 kila siku ukazitumia vizuri zinatosha kabisa.

3. Usikate tamaa, ukishindwa swali, muulize mwenzako, ikishindikana kabisa miongoni mwa wanafunzi wenzako, muone mwalimu akusaidie. Lakini pia, ukishindwa leo, jaribu kesho, keshokutwa nk. Hii njia itakusaidia, na hakuna kitakachokushnda.

4.hakikisha kabla ya kufanya mtihani wako wa taifa, Mock nk, uwe umefahamu mada nyingi kuanzia form 1 hadi 4. Usidharau topics ambazo huwa na maswali madogo madogo kwenye mitihani na kuwa na uzito wa maksi 3 hadi 6, hizo ndizo zitakusaidia kufikisha maksi nyingi. Wanasema "KIDOGO KIDOGO HUJAZA KIBABA". Kaa ukijua wanaotunga mtihani wa taifa hawajali kama umekamilisha mada au lah! Wale hawajua tabu watu wanazopata ktk shule za kata, kama vile kusoma topics 2 tu kwa mwaka mzima nk.

5. Kama wewe unaona haujafanya maandalizi ya kutosha, na hauna muda (mf. Form 4 kwa sasa wana takriban miezi 2), embu komaa na mada chache ambazo ni rahisi kwako kuelewa na utazipenda. Mf. Statistics, hii topic ipo kwenye hesabu na geograph, na hutoka section B (10 marks) hivyo ukiielewa vzuri utafaidika mara 2. Hapa ongeza na topics nyingine 2 au 3 ambazo hutoka section B, na unaweza kujiokoa na F. Unaweza kutafuta mtu wa kukusaidia ktk topics ulizochagua.
 
Last edited by a moderator:

Umenena ukweli mtupu!!! watu wengi wanakazana kufanya maswali hata mia kwa siku lakini ile mentaliti waliyoijaza vichwani ya "hesabu ni ngumu" inawakosti bila kusahau kitu kikubwa ulichokielezea hapo juu "KUIPENDA HESABU", lazima ukubali kwamba wanafunzi wengi wanaichukia hesabu!!!

Na kama ukiichukia hesabu au mwalimu wa hesabu(Hii ina apply pia kwenye masomo mengine) ni ngumu sana kufaulu hesabu!!! HII NIMESHAJIONEA KATIKA MAISHA YANGU YA KIELIMU NA BAADA KUJIREKEBISHA, SASA NAFURAHIA ULIMWENGU WA HESABU!!! Kudos to u for your productive post!!!
 
Tatizo watu tangu wakiwa shule za misingi, wanajengewa hyo hofu juu ya hesabu. Kuanzia wazaz hadi jamii inayotuzunguka inachangia wanachangia kuwaaribu watoto wao. Mzazi anadiriki kukiri mbele ya wanawe kuwa hesabu ni janga la taifa, sasa huyo mwanae atafanyaje?
 
Back
Top Bottom