Third Eye
JF-Expert Member
- Jan 8, 2012
- 373
- 210
Habari za asubuhi wanajamvi.
Nimekuwa nikitafakari sana hali ya kisiasa nchini. Ni ukweli ulio wazi kuwa Chama tawala (CCM) ni chama kikubwa, chenye rasilimali watu na fedha pamoja na kufanya kazi kwa ukaribu na vyombo vya ulinzi na usalama, bila kusahau tentacles zake ziko kwenye kila eneo la serikali. Hizi ni facts, ni hali halisi kwa ground ambazo hatuwezi kupingana nazo au kujidanganya kuwa hazipo.
Kwa kutambua hilo, mbinu zozote za kupambana na CCM ni lazima zijumuishe ukweli huo. Ningependa kupata mawazo ya wadau, kama una mbinu yoyote inayozingatia hali halisi niliyoeleza tushauriane hapa. Mimi naanza na moja;
Kwa kuwa CCM ina watu kwenye vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na serikali, nashauri vyama vya upinzani navyo kuanza ku-recruit au kupandikiza watu huko. Mfano, kunapotokea kuna ajira za polisi/TRA/Uhamiaji nk...vyama vya upinzani vichukue jukumu la dhati kuhakikisha kuwa vijana wa chama, wenye imani na vyama hivi wanapata nafasi hizo. Kuanzia kwenye kuhimiza wajiunge mpaka ku-lobby pale inapowezekana ili navyo viwe na watu wao huko.
Je, wewe unashauri mbinu gani itumike kuidhoofisha CCM na/au kuimarisha vyama vya upinzani?