Mbinu za kuona fursa na kuifanya biashara afrika

Mbinu za kuona fursa na kuifanya biashara afrika

Mzalendowadamu

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2016
Posts
218
Reaction score
318
Habari wana bodi. Leo naanza mfululizo wa Masomo ambayo napenda tujadiliane pamoja. Kabla ya kwenda mbali napenda niwaeleze kuwa ninayo yaandika hapa ni mawazo yangu kutokana na uzowefu wangu. Kama kuna nadhalia zozote za kiuchumi na mengineyo ya darasani basi endelea nayo mimi sipo kupinga hayo bali kuleta uzowefu wangu. Nitaeleza kwa uchache sana na kila jambo nitakua naliandikia mada kwa kina kadili nipatapo nafasi au uhitaji utakao kuwepo.

Ninatoa mbinu hizi kama msingi wa kukufanya uzione fursa za Ujasiriamali na Biashara katika nchi zetu za kiafrika.
Ujasiliamali ni nini? Mimi neno hili nalielewa kama ni hali ya kuwa na ubunifu unao lenga kutatua ugumu wa hali flani ya kimaisha katika jamii au mtu mmoja mmoja. Biashara mimi naelewa kuwa ni namna ya kuendesha shuguli flani ili iweze kutoa matokea chanya yatakayo saidia kuboresha maisha ya muendeshaji au/ na jamii. Jambo la muhimu kuelewa ni kwamba Ujasiriamali ili uwe natija lazima upate kuendeshwa kibiashara na hivyo kuwa zao ligusalo jamii pana zaidi.
Baada ya Utangulizi huo sasa tuendelee na mada yetu ya namna ya kuziona fursa katika afrika na kuzitekeleza.

1.Itambue vema jamii yako. Itambue kabila lako na tabia zake, wilaya, mkoa, kanda na mwisho itambue vema nchi yako , hapa ninamaana kijamii mila, desturi na Siasa .

2.Itambue Jiografia ya nchi, mko na wilaya yako.

3.Tambua na jifunze kuhusu Bara la afrika kijiografia ,kijamii na Siasa.

4.Jifunze kuhusu Mabara ya dunia kijiografia, kijamii siasa na Mahusiano.

5.Linganisha maendeleo ya Teknolojia na kijamii baina ya wilaya,mikoa, nchi na Mabara ya duniani.

5. Jifunze Lugha angalau moja ya Kimataifa na hasa Kiingereza na sio lazima ujue sana.

6.Tenga Muda wa kujifunza mambo unayo tarajia kufanya. Jifunze kupitia mtandaoni hasa google ili ujue ABC za hilo jambo.

7.Tangeneza Marafiki wenye maono kama yako, sio lazima kuwa nao karibu saana ila usipoteze mawasiliano yao.9kuna mbinu za kumvutia mtu wa maana awe rafiki yako)

9.Jifunze na zowea kuingia na kujieleza shida yako katika ofisi za mamlaka za serikali (hapa kujua Lugha kama Kiingereza huongeza kujiamini), pia jieleze kwa kutulia na tumia maneno ya kiofisi zaidi bila kusahau uvaaji.

10.Usitegemee kufuatwa kwa sheria kwa usahihi asilimia miamoja , wakati Mwingine kuna mazingira huhitaji kupata busara za wasimamizi wa sheria, Sheria nyingi sio rafiki kwa biashara katika nchi za Afrika lakini ugumu huo huzalisha mbinu flaniflani.Ugumu mwingine hutengenezwa makusudi ili mkutane pahala. Ukikuta ugumu pahala flani basi ujue iko namna hujaijua maadau wenzako wanaendelea na biashara. Pia tegemea kuwa wapo maafisa flani hawapendi ufuate sheria ili mkutane pahala flani. Mara zote huwa wanayo majibu sasa ni wewe kuongea nao kijamii zaidi( hapa namba 9 itakusaidia pia)

Kwa leo naomba niishie hapa. Kila Jambo hapo juu ni Mada inayo jitosheleza na tutazichambua moja baada ya nyingine. Kamaunayo maoni juu ya jambo lolote basi yaweke hapa au uliza swali lolote ili wakati wa kuchambua kiundani basi na swali lako liweze kupatiwa jibu.
 
Nadhani hii site ya ajiras.com inaweza saidia kwenye kujiajiri. Yenyewe inaruhusu mtu yoyote kuregister (bure) na kuuza huduma. Huduma ni ishu yoyote unayoweza kufanya. Kuwaandikia watu CV, kuchoma ndafu kwenye sherehe, kuandika business plan, kusajilia watu kampuni yaani kila kitu.
Bado impya ila ikichangaya hii, itatuvusha wengi sana. Inaitwa ajiras.com
 
Back
Top Bottom