Kama una afya nzuri ya mwili na akili kijana usiye na ajira unaweza kupata mtaji mdogo wa kuanzia, shida kubwa wengi wanafikiria kuanza na mamilioni, mimi nakupa wazo, kama huna ajira utakuwa unaishi kwa kutegemea mtu mwingine, ukiwa na uwezo wa kula na kulala bila kulipa anza kutafta vibarua, tunza pesa usitumie hadi ufikie malengo, tazamia miradi midogo inayofanywa maeneo yako, iga kama hunauwezo wa kubuni, utapata faida na faida hy itakupeleka kwenye lengo!nguvu zako ni mtaji na aibu yako ndiyo kikwazo kikubwa! Jishushe ipo siku utapanda