Mbinu za kutoboa Ozone enzi hizo tuko shule.

Youngblood

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
19,433
Reaction score
56,810
Maisha ya kusoma yana vituko vyake.

Moja ya vitu ambavyo havijawahi kufanya kazi kwangu wakati wa kusoma ni hii mbinu ya kuweka miguu kwenye beseni la maji, nakumbuka siku moja baba mdogo alinihadithia kwamba yeye wakati wake alikuwa anatoboa ozone kwa kutumia hiyo njia,siku moja nikaona isiwe tabu acha na mimi nikajaribu kama ni kweli , basi asikwambie mtu nusu saa haikupita nikapitiwa na usingizi mzito balaa, nimekuja kushtuka daftari zinaelea kwenye maji.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].

Mbinu pekee iliyokuwa inafanya kazi kwangu ni kutumia kahawa, nakumbuka nilikuwa natumia africafee kile kipact kidogo,kabla ya kwenda kutoboa, basi kuna kipindi nilifululiza kama week mbili natoboa tu,siku moja naingia prepo nikaanza kuona maruweruwe ikabidi nijipe likizo ya kusoma kama week.[emoji1787][emoji1787][emoji1787].
 
Hizo za kwenye maji tumetumia sna, tena unapanda Nayo dekan olewako usinzie ummwagie alioko chini utajutraaaa
 
Watu tulikunywa kahawa na bado tukawa tunalala

Kufeli ni ka process kanaanzia mbali sana

Kahawa na bado unalala kupitiliza na adhabu juu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dah mkuu wewe ulikuwa na ugonjwa wa kulala
Watu tulikunywa kahawa na bado tukawa tunalala

Kufeli ni ka process kanaanzia mbali sana

Kahawa na bado unalala kupitiliza na adhabu juu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Katika vipindi vigumu wanavyopitia waafrika ni pamoja na maisha ya shule
 
Balaa la kuweka miguu ndani ya maji lile baridi la saa nane unalisikia mpaka mgongonii
 
Kuna jamaa wao walikuwa wanatumia ugoro ..then baada ya hapo lazima wakakeshe kwa class hadi asubuhi
 
Dah...Sijawahi kutoboa hata siku moja[emoji2960]
 
Kuna kipindi nilipiga matundu kama wiki nzima mfululizo, nikawa nasikia moyo unataka kuchomoka.

Ukubwani huku tunapiga matundu kwa mawazo tu, unakuta unawaza hela ya kodi, mkopo wa board, makato ya saccos, ada za watoto, tuition fee ya wadogo, na hela ya wazazi. Ukiwaza yote hayo usingizi hauji na dushe linalala.
 
Nakumbuka advance kuna jamaa alikuwa mtoboa ozone mzuri sana.

Yani wewe ukienda prepo saa moja yeye utamkuta kashaanza kitaambooo. Unaondoka unaenda kulala, ukiamka saa 10 unamkuta yeye kashaamka kitaambooo anakula msuli bed.,[emoji23][emoji23][emoji23]

Unforgetable
 
Hao watu kila kwenye shule hawakosekani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…