Efendi
JF-Expert Member
- Aug 23, 2016
- 314
- 438
MBINU ZA NATIONAL AL AHLY HIZI HAPA.
-Kwa kuwekeza muda wangu wa siku kama tatu ivi kwa kufanya tafiti za kisayansi juu ya mbinu za al ahly katika michuano ya Afrika.
Ikiwa Ugenini.
-Sifa kubwa ya Ahly wakiwa ugenini ni Mbinu mbili tu, Msingi wao mkubwa ni kumheshimu Mpinzani akiwa Kwake. Wanauzoefu Mkubwa sana wanajua soka la afrika timu ikiwa nyumbani hucheza vema hata kama ni dhaifu (Underdogs).
-Kwanza Hutumia Dakika kama 10-15 za mwanzo kushambulia kwa kasi kubwa, Lengo kubwa ni kutest mitambo kwa Mpinzani, Je ukimshambulia kwa kasi anafungika ? Udhaifu wao upo wapi ?
-Kama Timu mwenyeji ikiwa dhaifu katika mbinu hiyo Yaani wameshindwa kuwazuia wanakufumua hapo hapo kwako. Kama wakigundua kufunguka kwao kunawaponza kitu Fulani kama Mwenyeji anakua na nidhamu nzuri basi na wao wanaacha hiyo mbinu wanarudi nyuma wote.
-Mbinu ya kwanza imefeli, mbinu ya pili ni kucheza Deep (Ukinzi) alafu wanatengeneza Mashambulizi ya kustukiza, Hutumia aina mbili za Counter attack Solo au Classic counter attack.
-Mtu nambari moja katika kuanzisha hizo counter attack kwa sasa ni Walid Soliman, huyu akipata mpira humpelekea Striker wao Walid Azarou huyu Jamaa huwa na utulivu sana katika mipira hiyo, na Mara nyingi huwa anaweka kambani au anamfata mlinzi ili ajiangushe.
-Zingatia: al ahly Faulo (Free kick) kwao wanaweka 70% kua ni goli, kama huamini fuatilia mikanda yao ya ugenini kwenye ligi hii. Ingia You tube andika Al ahly vs Orlando pirates CAFCL final 2014. Utaona, kisha andika Yanga vs Al ahly 2016. Utaona nnachomaanisha.
-Ikitokea wamekufumua Goli moja tu, hata kama kuna uwezekano wa kuongeza goli huwa wanarudi nyuma na kulinda goli lao, Huku wakiimaliza hiyo game kwa namna moja hii ukiwa umeamka mwishoni unawashambulia kwa kasi huwa wanaanguka kama Malwedhe challenge, wanaimaliza mechi ataanguka kipa ili kumkata moto mpinzani huku Wachezaji wanakimbilia kwa mwalimu kupata maelekezo.
-Mara nyingi hucheza Dk 70-75 game za ugenini, Muda mwingi wanalala ovyo, Zaidi wakishinda.
Mwisho: Wakiwa kwao usitarajie kuona mtu analala, Wanazitamani dakika zaidi ya 90 na mpinzani akilala wakati ambao wao hawajapata Matokeo mazuri huwa wanamlazimisha mwamuzi na madaktari aende nje huyo Mchezaji. Pia Kwao huwa hawazuii kama mpinzani ni imara basi atoke kwake aende akafunge, wanakuapa nafasi sasa jaribu kufunguka uone kitakachokukuta.
-Pamoja na hilo Mashabiki wao Huwa wanamaliza Mchezo mapema sana, Wanawasha Baruti uwanjani, Wanamulika Tochi za rangi usoni wapinzani, Hubeba bendera, wanaimba na kuruka ruka wakiwa wameshikana mabegani, (Tifo style). Hawapoi.
Mtazamo tu.
-MWL. WILLIAM
Sent using Jamii Forums mobile app