Mbinu za National Al Ahly hizi hapa

Mbinu za National Al Ahly hizi hapa

Efendi

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2016
Posts
314
Reaction score
438
MBINU ZA NATIONAL AL AHLY HIZI HAPA.

-Kwa kuwekeza muda wangu wa siku kama tatu ivi kwa kufanya tafiti za kisayansi juu ya mbinu za al ahly katika michuano ya Afrika.

Ikiwa Ugenini.

-Sifa kubwa ya Ahly wakiwa ugenini ni Mbinu mbili tu, Msingi wao mkubwa ni kumheshimu Mpinzani akiwa Kwake. Wanauzoefu Mkubwa sana wanajua soka la afrika timu ikiwa nyumbani hucheza vema hata kama ni dhaifu (Underdogs).

-Kwanza Hutumia Dakika kama 10-15 za mwanzo kushambulia kwa kasi kubwa, Lengo kubwa ni kutest mitambo kwa Mpinzani, Je ukimshambulia kwa kasi anafungika ? Udhaifu wao upo wapi ?

-Kama Timu mwenyeji ikiwa dhaifu katika mbinu hiyo Yaani wameshindwa kuwazuia wanakufumua hapo hapo kwako. Kama wakigundua kufunguka kwao kunawaponza kitu Fulani kama Mwenyeji anakua na nidhamu nzuri basi na wao wanaacha hiyo mbinu wanarudi nyuma wote.

-Mbinu ya kwanza imefeli, mbinu ya pili ni kucheza Deep (Ukinzi) alafu wanatengeneza Mashambulizi ya kustukiza, Hutumia aina mbili za Counter attack Solo au Classic counter attack.

-Mtu nambari moja katika kuanzisha hizo counter attack kwa sasa ni Walid Soliman, huyu akipata mpira humpelekea Striker wao Walid Azarou huyu Jamaa huwa na utulivu sana katika mipira hiyo, na Mara nyingi huwa anaweka kambani au anamfata mlinzi ili ajiangushe.

-Zingatia: al ahly Faulo (Free kick) kwao wanaweka 70% kua ni goli, kama huamini fuatilia mikanda yao ya ugenini kwenye ligi hii. Ingia You tube andika Al ahly vs Orlando pirates CAFCL final 2014. Utaona, kisha andika Yanga vs Al ahly 2016. Utaona nnachomaanisha.

-Ikitokea wamekufumua Goli moja tu, hata kama kuna uwezekano wa kuongeza goli huwa wanarudi nyuma na kulinda goli lao, Huku wakiimaliza hiyo game kwa namna moja hii ukiwa umeamka mwishoni unawashambulia kwa kasi huwa wanaanguka kama Malwedhe challenge, wanaimaliza mechi ataanguka kipa ili kumkata moto mpinzani huku Wachezaji wanakimbilia kwa mwalimu kupata maelekezo.

-Mara nyingi hucheza Dk 70-75 game za ugenini, Muda mwingi wanalala ovyo, Zaidi wakishinda.

Mwisho: Wakiwa kwao usitarajie kuona mtu analala, Wanazitamani dakika zaidi ya 90 na mpinzani akilala wakati ambao wao hawajapata Matokeo mazuri huwa wanamlazimisha mwamuzi na madaktari aende nje huyo Mchezaji. Pia Kwao huwa hawazuii kama mpinzani ni imara basi atoke kwake aende akafunge, wanakuapa nafasi sasa jaribu kufunguka uone kitakachokukuta.

-Pamoja na hilo Mashabiki wao Huwa wanamaliza Mchezo mapema sana, Wanawasha Baruti uwanjani, Wanamulika Tochi za rangi usoni wapinzani, Hubeba bendera, wanaimba na kuruka ruka wakiwa wameshikana mabegani, (Tifo style). Hawapoi.

Mtazamo tu.

-MWL. WILLIAM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kuvuta bange kwa kisingizio cha kujifanya mchambuzi wa mpira

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mbona waliondoka bila point kwenye World cup, Wanajua mpira au figisu

Hakuna cha figisu wala nini, Mungu amewapa kipaji waarabu..sio akina sisi kelele nyingi uwanjani SIFURI .Kuhusu w/c bora yao wanashiriki, je sisi tushawahi? Hata mashindano ya Afrika tu je tushawahi!!!
 
Sisi hatujui mpira na hatutokuja kujua, ila hii haiwafanyi Waarabu kujua mpira zaidi ya figisu
Huanza kudiscorage timu pinzani toka inapowasili airport, hujuma mahotelini, kuathiri wapinzani kisaikolojia na uwanjani wanakwenda kumaliza kwa kikufunga, kama wanajua mpira kuna haja gani ya hayo mengine? Figisu za hawa jamaa zinajulikana si tu kwa timu za Ukanda wa Afrika mashariki bali Afrika nzima
 
Hakuna cha figisu kamanda, inshort wale sio wenzetu bwanaa...je waweza weka kithibitisho kuhusu unachokiongea! Ili sote tupate kujuwa kama nikweli! Au comments za mitandaoni kwa akina shaffi dauda/edo kumwembe ndiyo zimekufanya uamini hivyo? Pole sana....
 
Sisi hatujui mpira na hatutokuja kujua, ila hii haiwafanyi Waarabu kujua mpira zaidi ya figisu
Huanza kudiscorage timu pinzani toka inapowasili airport, hujuma mahotelini, kuathiri wapinzani kisaikolojia na uwanjani wanakwenda kumaliza kwa kikufunga, kama wanajua mpira kuna haja gani ya hayo mengine? Figisu za hawa jamaa zinajulikana si tu kwa timu za Ukanda wa Afrika mashariki bali Afrika nzima
Mkuu waarabu wanajua quraan na kutumia jambia.mpira wanajua fitina tu.
 
Hao huwa wanashinda kwa fitna tu hakuna jingine. Ndio maana hata timu zao zikicheza michuano mikubwa nje ya Africa wanageuzwa jamvi.
 
Kwani fitina sisi hatuwezi, Mpira hatujui na figisu pia.
 
Hivi wale marafiki zangu wapenzi wa Simba NGUVU MOJA ina maana huu uzi hamjauona. Wacheni hizo basi. 😀😀😀
 
Hao huwa wanashinda kwa fitna tu hakuna jingine. Ndio maana hata timu zao zikicheza michuano mikubwa nje ya Africa wanageuzwa jamvi.
Ya kweli haya Mtani? Kwa nini na sisi hatuzifanyi hizo fitna sasa?
 
Back
Top Bottom