Mbinu za siri za kuishi Tanzania bila kuteseka

Naongezea;
Usimsimange boss wako;
Usimshirikishe yoyote mambo yako ya siri Hasa kuhusu utafutaji na riziki.
Fanya ibada.
Usiishi uswahilini sana utarogwa.
Usitembee na mke wa mtu hata akikutaka ,wala usijenge mazoea nao.
Ishi kulingana na pato lako.
Usitegemee marafiki wa ki tz wakusaidie kwenye njaa.
Jenga utaratibu wa kufanya saving.
Kaa mbali na vitu kama mirathi,uwe wa mwisho kuongeza.
Ukienda ugenini usiwe na pupa ya marafiki wapya,somo game kwanza.
Machawa wasikilize ,ila usifanya maamuzi kwa maneno yao.
 
Kwahiyo wewe mjinga maisha ni kula kunywa na kulala

Wajinga Kama nyie ambao mnaamini maisha ni kujairiwa serikalini kula kuvaa na kupata pango sehemu ya kuegesha mbavu mnazingua Sana
Mkuu bado hujaleta hoja naona unaghadhaba, wewe maisha yanawexa yakawa magumu sanaa ila haimanishi kwamba ni magumu kwa kila mtu, ukweli ni kwamba Tanzania ni nchi nyepesi kuishi bila kutumia akili sanaa labda kama una kasoro zako personally
 
Mkuu mbona 60,000 ni mbonge la pesa mtu anapata 30,000 kwa mwezi ila nakitambi anacho maisha hapa Tanzania ni mepesi sanaaa angalia idadi ya wa piga debe pale mbezi magufuli wote wanapata Rizki ya kutosha.


Inawezekana una exposer ndogo au kwa makusudi umeamua kufurahisha genge

Kama kula ilimradi umekula upo sahihi

Ila watanzania aslimia kubwa wanasukuma siku na sio kuishi

Huwa nashangaa sana mtu akisema Tanzania ina nafuu ya maisha itakuwa anafikiria maisha ni kula chochote , kulala popote na kuvaa chochote ila sio standard life.

Tanzania ili uwe na standard life is not easy hasa ukiwa unafanya shughuli halali.

Maneno kama yako huwa wanayaongea waajiriwa ambao wanatafutiwa ugali na mwajiri wao na sio kwa watu ambao wapo field wanapambana na maisha .
 
Ukizaliwa Afrika automaticaly tayari maisha yashakupiga goli 1-0, kama hauna connection 2-0, ukioa 3-0. Hapo upige comeback shughuli yake sio ya kitoto
 
Mkuu wewe unategeme mpiga debe au muendesha bajaj ajenge ghorofa kwanza ndo yawe maisha mazuri? Neenda South Sudan robo ya raia wanalala nje hawana shelter wana kula mara moja neenda Ethiopia ujionee hata kupata kazi ya mpiga debe haipo.
 
Ukizaliwa Afrika automaticaly tayari maisha yashakupiga goli 1-0, kama hauna connection 2-0, ukioa 3-0. Hapo upige comeback shughuli yake sio ya kitoto
Ni kweli mkuu! Mfano mzuri ni mtu anayekulia kijijini bila connection , anaanza maisha akiwa tayari nyuma. Akimaliza shule hana ajira kwa sababu kazi nyingi zinapatikana kwa "mtu wangu yupo." Akioa mapema bila kuwa na msingi imara kifedha, majukumu yanaongezeka maradufu. Hapo comeback yake inahitaji akili, juhudi, na uvumilivu wa hali ya juu!
 
Aah kwani ungenena bila mafumbo tusingeelewa mkuu?
Kuna faida ya kutumia mafumbo. Moja ya faida ni kwamba concept inaeleweka kwa kina zaidi kuliko kusema moja kwa moja. Mafumbo yanachochea fikra, yanahimiza tafakuri na yanasaidia ujumbe kupenya kwa namna ya kipekee zaidi. Wanaojua, wataelewa haraka; wanaotaka kujua, watatafuta maana na hapo ndipo ujumbe unakaa kwenye akili zao kwa muda mrefu.
 
Tanzania na uenda Afrika kwa ujumla tumeshakua addicted na maisha ya shida kiasi kwamba tunaona huo ndio ustaarabu wa maisha ya binadamu.

Kwetu ufukara tumeutengenezea picha kama taswira ya uadilifu, uzalendo na hadhi nzuri. Haishangazi hata JPM alipata mashabiki wengi sana kwa kujiita Rais wa wanyonge.
 
Na iyo comeback inaweza iaifanyike kabisa. Matokeo yakabaki ivyo ivyo au maisha yakakupiga chuma cha 4
 
Ukishindwa kuishi Tanzania kwa neema zake naupesi wa maisha usijaribu kuenda Kenya Zibabwe Ethiopia na nchi nyingi kabisa, ukweli ni kwamba Tanzania unaweza ukaishi popote bila kutumia nguvu nyingi kabisa.........
Huko Kenya kuna matajiri, na watu wana kula bata si za kitoto..

Acha woga wako ndio umaskini wako.
 
Na kila tajiri akamwita ni mpiga madili akaanza kumshughulikia. Akapoteza lengo la kuwaletea wananchi maisha bora akaishia na udikiteta tu
 
,πŸ‘ŠπŸΌ
 
Na iyo comeback inaweza iaifanyike kabisa. Matokeo yakabaki ivyo ivyo au maisha yakakupiga chuma cha 4
Hapo ndo changamoto kubwa! Unaweza pigana comeback kwa nguvu zote, lakn kama mazingira hayabadiliki au mfumo unakukandamiza, unaweza jikuta matokeo yanabaki vile vile bora liende. Mbaya zaidi, ukijikwaa vibaya, maisha yanakupiga goli la 4, unakuwa officially umetoka kwenye game. Ndy maana comeback inahitaji siyo tu juhud, bali pia mbinu sahihi, bahati kidg, na connection za maana!
 
Mkuu sijaelewa hoja yako hapa unacho maanisha ni nini hasa, kwamba Tanzania ni ngumu sanaa kuishi au?
Baadhi ya maeneo ni ngumu sana kuishi, kwa mfano nenda Musoma mara ule mji mzunguko wake wa pesa unaendeshwa na upatikanaji wa samaki na dagaa, kipindi Cha Giza pesa ipo na inapatikana na wepesi ila kipindi Cha mbaramwezi mambo yanakuwa magumu sio kwa wauza nguo au wauza vyakula, Mimi nimeishi sehemu nyingi sana Tanzania hii
 
Kenya ni nyoko kule amna mamb yakuombana chumvi/unga kule ndo ubepari Sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…