Mbinu zipi za ziada za kupata utajiri kwa njia halali kabisa?

SAYANSIKIMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2014
Posts
1,132
Reaction score
260
Ujue baadhi ya matajiri waliofanikiwa kutoka kimaisha ni wajanja sana Wanaficha FORMULAR walizotumia ilikufanikiwa .

Kuna wengine ukiwauliza ulitokaje kimaisha wanasema FANYA KAZI KWA BIDII lakini wapo watu wanaojituma kuchapa kazi kwa bidii lakini hawajafanikiwa .Wengine wanasema jipange usikate tamaa utafanikiwa tu ,mara kazana kusoma ,mara nenda kwa mganga fulani lakini wengi wanafanya hayo lakini bado hawajafanikiwa maisha bado magumu tu.

Huwa najiuliza hawa matajiri wenye hela na malinyingi sana ambao kipindi cha nyuma walikuwa na maisha magumu au ya kawaida walifanya nini cha ziada .Maana kwa kweli hata mimi napenda mbeleni nitoke kimaisha lakini nafikiria na kupanga mipango na huwa na rekodi mipango katika maandishi na kuisoma lakini bado maisha ya kawaida .

Nyie mliofanikiwa mlifanya kipi cha ziada tupeane mbinu basi maana na mimi na penda kipindi cha mbeleni nitoke kimaisha .Mlitumia NJIA NA MBINU GANI ZA ZIADA.
 
MBINU:

A) Uwe mbunifu wa mambo madogomadogo na Mungu atakuinua kwa makubwa
B) Usipende kulala yaani usiwe mvivu fanya kitu ili kiwe historia ya maisha yako kwa kizazi chako cha baadaye
C) Uwe mwenye bidii, juhudi na mstahimilivu kwa wakati bado unaangaika na maisha usiwe mwenye tamaa
D) Usipende maisha ya SHORTCUT kwani sio mazuri yatakuletea balaa na majanga bure
 
Fuata sheria za laws of attraction hiyo ndio formula.
 
Mbinu ya kwanza ni kubana matumuz(2)kuweka akiba(3)kufanya kaz kwa bidii bila kukata tamaa na mwisho mshirikishe mungu kwa kila jambo utafanikiwa.
TEMBELEA HUMU MAANA NDIMO KUNA UTAJIRI. ...!!

1. Tafuta vyanzo mbalimbali vya mapato, hakuna mtu anayetoka kirahisi kwa kutumia chanzo kimoja
2. Usiogope mikopo
3. Ujifunze kubana matumizi - siri kubwa ya kutoka ni kubana matumizi
4. Mtangulize Mungu katika kila jambo

Anza na kilimo. Tefuta eneo lenye uhakika wa maji. Tumia nguvu na maarifa ulivyojaliwa taratibu utapata mtaji na utabuni zaidi cha kufanya
 
utajiri ni njia mbili tu mkuu
1.kubahatika kupata nafasi ya kukupa utajiri
2.kua na mipango madhubuti ya kuitumia bahati hiyo
kwasababu wapo watu wanahangaika sanna ila hawajabahatika kupata nafasi hiyo
ila pia wapo wale ambao wanapata nafasi ila hawaifanyii kazi wanaipoteza
ila wapo ambao wamepata nafasi na wamejipinda kuifanyia kazi
nnachomaanisha hapa jipinde kadri ya uwezo wako huwezi jua nafasi ya bahati yako ipo ktk nyanja ipi
 
Hata matajiri ukiwauliza walitokaje wanaweza wasikupe jibu la moja kwa moja.

Fanya haya yatakusaidia.

* omba zari la mentari likutokee.

Hasikuambie mtu kufanikiwa ni bahati na rehema za Mungu.

Pili ziko tabia zitakazokusaidia kumentain status ya utajiri.
1: kuwa na nidhamu ya pesa.
2: jitume kwa bidii yote ukiluhusu ubunifu; kutokukata tamaa; penda kujifunza....!


Kwangu mimi mtu kuwa tajiri hainipagi shida sana ila unataka ufanye nini na huo utajiri hapo ndo patamu.


Kumiliki majumba; magari ya kifahari na aina zote za kula bata yaone tu watu wakiigiza maisha hayo ila ukipata mtu honest akusimulie hao walio na maisha hayo ni kwa kiwango gani wanafurahia maisha yao
Cku hiyo utazimia.
Asimilia zaidi 98% ya matajiri hawana furaha na maisha yao yamejaa hofu na mashaka tele.


Kumbe jambo bora ktk maisha ni Mungu akupe life purpose ambalo litaleta maana ya maisha na furaha.


Hivyo badala ya kutamani sana kuwa tajiri plz tamani sana kujua upo duniani kufaya nini.
 
point mkuu
 
1. Tafuta vyanzo mbalimbali vya mapato, hakuna mtu anayetoka kirahisi kwa kutumia chanzo kimoja
2. Usiogope mikopo
3. Ujifunze kubana matumizi - siri kubwa ya kutoka ni kubana matumizi
4. Mtangulize Mungu katika kila jambo
point mkuu
 
Mimi mwenyewe nipo hapa kusikia matajuri watatujibu nini, maana nimekomaa sana lkn bado pagumu.
 
Utajiri wa kweli ni usafi wa Roho yako, hayo mengine ni mbwembwe tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…