Tanzania Nchi Yetu Sote
JF-Expert Member
- Mar 12, 2017
- 505
- 872
Maeneo yanayopitiwa na mbio za mwenge wananchi wanateseka bila sababu. Chukulia mfano leo mwenge ulikuwa unaenda kuzindua barabara iliyojengwa kiwango cha zege kuanzia eneo linaloitwa sauzi mpaka matosa kuelekea njiapanda ya goba. Cha kushangaza barabara ilifungwa tangu jana kuanzia msikiti mdogo bila sababu yoyote ya msingi. Leo asubuhi ikawa ni mateso matupu kwa abiria. Uzinduzi unafanyikia matosa lakini kuanzia msikiti mdogo mpaka njiapanda ya goba kumefungwa. Vijana wasiovaa sare wametundika pingu viunoni na kushika radio calls mikononi walikuwa wakiwaonesha cha mtemakuni bodaboda waliokatiza.
Mwenge usigeuke kero kwa kuchelewesha watu kujitafutia riziki zao.
Mwenge usigeuke kero kwa kuchelewesha watu kujitafutia riziki zao.