Simba wawe waangalifu sana kwani kuna suala la "goal difference" linaweza kujitokeza mwishoni mwa ligi kwani ligi ya mwaka huu ni moto weka mbali na watoto. Niwakumbushe tu viongozi na benchi la ufundi kuwa msimu wa 2016/2017
Simba na Yanga walikuwa na pointi 68 lakini Yanga akachukua ubingwa kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa kwani Yanga alikuwa na magoli 10 zaidi ya Simba..
Sasa ninaposema Simba wawe waangalifu sana ni kwa sababu Simba kuna muda wanakuwa wameizidi timu pinzani kwa kila kitu lakini wakishafunga magoli mawili/matatu basi mchezo unaishia hapo hakuna ladha tena ya kutizama mpira kwani wachezaji wanaridhika wanaanza kupigiana pasi fupi fupi badala ya kutafuta magoli zaidi. Mfano mzuri mechi ya jana na Prison kiukweli Simba walikuwa na uwezo wa kushinda hata goli 7 kama wangedhamiria. Lakini walipopata magoli matatu wachezaji na benchi la ufundi wakaridhika wakamuingiza Deborah ambaye muda wote alikuwa anapiga pasi za nyuma badala ya kwenda mbele ili timu ipate magoli zaidi.
Aliye karibu na Mo Dewji, viongozi wa Simba na hata benchi la ufundi awakumbushe hili mapema wawambie wachezaji wao wafunge magoli kadiri wawezavyo ili mwishoni mwa ligi wasije wakapata presha na kujutia. Wenzao Yanga hawarembi mtu akiingia kwenye mfumo anakula 5 au 6 kwani wanajua nini kilitokea msimu wa 2016/17. Ikiwezekana benchi la ufundi la Simba na wachezaji wote wa Simba wakiwa mapumzikoni kambini waonyeshwe msimamo wa ligi ulivyokuwa msimu 2016/17 labda akili zao zitawakaa sawa na labda wataacha mambo ya "show game" na kuanza sasa kutafuta mtaji wa magoli.
Ni mtizamo tu