Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Infaltion inafanya maisha yanakuwa magumu sana. Athari kubwa zinakuwa upande wa lishe. Si vema kupata utapiamlo na hali unaweza solve kwa kuotesha mbogamboga hapo nyumbani. Tushirikishane juu ya mbogamboga na vyakula vingine ambavyo mtu anaweza kuzalisha nyumbani.
1. Kisamvu. Hapa nazungumzia ile miti ya kisamvu ambayo huwa mikubwa sana na haitois mihogo. Badala ya kupanda miti ya mapambo basi panda huu mti. Ukipata maji unatoa mboga mwaka mzima.
2. Badala ya kupanda maua panda nyanya chungu. Hizi zinazaa mwaka mzima. Pia matunda na majani yake vyote ni mboga nzuri, so unavyosubiria matunda unakuwa unapata mboga za majani.
3. Otesha hoho. Pilipili hoho ukitunza vizuri zinazaa kwa muda mrefu sana.
4. Panda matembele. Matembele huwa yanadumu sana. Umwagilie tu.
5. Hata nyanya unaweza panda na kuepuka. Itakusaidia pia kuepuka zenye madawa.
Mazao hawa unazalisha hata kwenye makopo. Si mpaka uwe na eneo kuuubwa.
6. Chakula gani kingine mtu anaweza kuzalisha nyumbani?