Naomba kufahamishwa ukweli, nimekuwa nasikia mitaani kuwa ulaji wa mboga za majani aina ya Kabichi siyo mzuri kwa afya kwa watu wenye ugonjwa wa Goita.
Mimi kama mdau wa mboga za majani huwa napata wasiwasi sana juu ya maelezo haya. JamiiForums naomba mnisaidie kujua ukweli wake.
Nawasilisha.
Mimi kama mdau wa mboga za majani huwa napata wasiwasi sana juu ya maelezo haya. JamiiForums naomba mnisaidie kujua ukweli wake.
Nawasilisha.
- Tunachokijua
- Goita (Goiter) ni uvimbe unaotokea kwenye tezi ya thyroid inayopatikana sehemu ya mbele ya shingo. Tezi hii yenye umbo linalofanana na kipepeo huzalisha homoni za T4 na T3 ambazo huhusika kwenye kuratibu mifumo mbalimbali ya mwili ikiwemo joto, mihemko ya mwili, mapigo ya moyo na mmeng’enyo wa chakula.
Mgonjwa wa Goita
Upungufu wa madini joto (Iodine) ndio chanzo kikubwa cha kutokea kwa ugonjwa huu. Wakati huu, tezi za thyroid huongezeka ukubwa ili kufidia upungufu uliopo, jambo ambalo huifanya ivimbe.
Sababu zingine kama uwepo wa kiasi kingi au kichache sana cha homoni za thyroid, maambukizi kwenye tezi za thyroid, saratani na ujauzito zinaweza kusababisha kutokea kwa Goita.
Baadhi ya dalili zake-
- Uvimbe shingoni
- Maumivu na Kukaza kwa shingo
- Ugumu kwenye kupumua na kumeza chakula
- Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
- Uchovu usio na sababu
- Kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi
- Sauti kuwa ya mikwaruzo
- Wakati mwingine, mishipa ya damu ya shingoni inaweza kuvimba pia na kusababisha mtu kujihisi kizunguzungu pindi anapoinua mikono yake juu
Pia, tumia chumvi iliyoongezewa madini haya kila siku. Unaweza kuitambua chumvi yenye madini haya kwa kusoma kifungashio chake kwanza kabla haujainunua.
Kabichi ni mbaya?
JamiiForums imefanya uchunguzi kwa kurejea tafiti mbalimbali, pamoja na kuzungumza na madaktari bingwa wa afya ya binadamu. Katika uchunguzi wetu, tumebaini mambo yafuatayo;
- Ni kweli kuwa mboga hii sio salama ikiwa itatumiwa kwa kiasi kikubwa na watu wenye ugonjwa wa Goita.
- Mboga zingine za majani zinazopatikana kwenye kundi kubwa la mimea ya Cruciferous ambamo kabichi hupatikana kama vile brokoli, Kale na cauliflower sio nzuri pia kwa watu hawa.
- Hupunguza uwezo wa tezi za thyroid kwenye kutumia vizuri madini joto (Iodine), hivyo kuongeza uwezekano wa kukua kwa tatizo.
Kwa mujibu wa Taasisi ya Mayoclinic, mgonjwa anaweza kutumia kiasi kidogo bila kupata madhara yoyote, pia inashauriwa kutumia walau saa 3 kabla au baada ya kumeza dawa za kutibu ugonjwa huu.