Hapana, sio sahihi!! Hata hivyo, Ali Kiba ameshapita level za kuzunguka na Fiesta! Yule angekuwa ni mtu wa kukaza alitakiwa awe ni mtu wa kwenda baadhi ya show tu lakini sio kila mahali!
Ningekuwa ndie meneja wa Kiba ningesema huyu level zake ni Arusha, Mwanza, Mbeya na Dar pekee lakini sio kuzunguka nae kwenye Coaster!
Na kama Diamond Platnumz atakuwepo Dar es salaam Fiesta, basi kama wanajitambua Kiba na management yake wanatakiwa kugomea hiyo show manake itaonesha wazi kwamba Diamond alikuwa reserved for the big show as a lead artist kama ambavyo zamani hao lead artists walivyokuwa wanatoka nje!