Tiketi ni za moto sana na maisha ya USA yapo juu mno ndio maana atuoni matangazo ya makampuni kutoa ofa ya watu kwenda kuona hata mechi moja
Tiketi ya bei chee ni 30m+ huu ni mtaji
Kwa sasa tiketi zimepungua bei sana. Kuna makala nilikuwa nasoma inaelezea hili.
Kuna dada mmoja Mtanzania alienda kuona mpira Boston mechi ya Ghana na England. Na kuna wengine wengi tu wameenda. Ila si kila mtu ana tabia ya kujionesha kwamba kaenda. Wengi tushapita stage ya kufanya mambo ili tujioneshe kwa jamii. Tunaona huo ni ulimbukeni.
Wengine tunaongea marafiki wa karibu tu hutawaona kujishaua ku post haya mambo kwenye mitandao ya kijamii. Wengine hata hawana accounts kwenye hiyo mitandao ya kijamii.Wewe huwajui Watanzania wote.
Pia, wengi mpira si fani yetu kihivyo, hatuelewi objectively umuhimu wa watu kufukuza mpira kuuingiza katika goli, katika dunia yenye matatizo mengi, ya kiuchumi, kijamii etc, na wengi hatupendi sehemu zenye kujazana watu yenye makelele mengi, tunaona hayo ni maisha ya kizamani, entertainment ya enzi za falme za Kirumi wakati watu hawakuwa na TV.
Si kila mtu anafanya kitu kwa kufuata mkumbo tu kama unavyofikiri wewe au kwa sababu watu wengi wanakifanya. Wengine hujiuliza sana umuhimu wa mambo kabla ya kuyakubali.
Mimi nilikuwa nafanya kazi katika kampuni inayo sponsor moja kati ya viwanja vinavyotumika zaidi ya miaka 22 iliyopita, they still have their brand on the stadium, na kwa sababu hiyo, nilikuwa napata nafasi ya kupewa tiketi kwenda kuona hii michezo, bure. Lakini sijawahi kufuatilia, hata siku moja, kwa sababu naona kwenda uwanjani kuangalia michezo ni ghasia tu kwangu. Si fani yangu.
Sasa hii si fani yangu, unataka leo ndiyo niende kushobokea mpira kwa sababu ni World Cup? Unafikiri ulivyo wewe kila mtu yupo hivyo? Unafikiri watu tunaishi kwa kufuata mkumbo?
Zaidi, kwenda uwanjani kuona mpira mara nyingi ni suala la "Status Anxiety" tu, mtu apate kujitapa kuwa alikuwapo uwanjani. Kwa sababu mtu anayekaa nyumbani anaweza kuuona huo mpira vizuri zaidi kutoka angles tofauti kwa kupitia TV akiwa kwake, akiwa anapata analysis, anapigwa na AC, anakula anachotaka, kuliko anayeenda uwanjani kupigwa na jua au mvua.
Kwa upande wangu hizo ni sababu muhimu zinazonifanya nisitake kwenda uwanjani hata ukinipa tiketi za bure licha ya kwamba uwanja mmoja upo kilomita chache kutoka ninapoishi.