Mbona Mbowe yuko kimya, ni kawaida yake?

Getrude Mollel

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2022
Posts
270
Reaction score
362
Kulingana na mfululizo wa matukio ya hivi karibuni yaliyotokea nchini, si kawaida kukuta kiongozi wa Chadema akikaa kimya kama ilivyo ada yake.

Duru mbalimbali zinasema kwamba Mbowe amesharamba asali tayari, ametulizwa. Hubu tusemeni jamani, ni kawaida ya mbowe hii kweli, hata tweet kweli? kweli?
 
kwani lazima Mbowe aongee?

chama kimeshatoa nsimamo

busara lazima itumike kulinda Maridhiano

hamkumbuki kina Maalim Seif baada ya maridhiano walianza hata kuhudhuria Sherehe za Mapinduzi Matukufu zilizohitimisha Tawala na maisha ya Babu zao



kuna majimbo 'tumekubaliana tayari na ndio sababu 'NURU NA BASHASHA' za Heche na Mchungaji Msigwa zimerudi
 
Mwacheni apumzike. Alishakaa Mahabusu kwa muda mrefu na anaogopa kesi ya ugaidi ikifunguiliwa tena. Unajua DPP alisema hana interest ya kuendelea na kesi hiyo kwa wakati ule, lakini haina maana kua alifuta kesi. DPP akiamua anaweza kuliamsha tena.
 
Nchi haiwezi kuwa kimya hivi. Tunaweza jikuta tumeuzwa wootee.
 
Mpigie simu🤔
 
Mbona nilimuona Jumapili akiimba kanisani, hapo ukimya uko wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…