Mbona Professor Jay hakupewa Uwaziri?

Mohammed wa 5

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2022
Posts
1,215
Reaction score
3,035
Hizi nafasi za Uwaziri zinatolewa kwa upendeleo au ukipata kama zali? Mbunge wa zamani Jimbo la Mikumi na Msanii mkongwe wa Hip-Hop Joseph Haule (professor Jay), alihudumia Bunge kwa miaka mitano ila hakupewa hata Uwaziri.

Kama sifa walizotumia kumpa Uwaziri Mwana FA mbona Professor Jay alikuwa nazo?

 
Mwana fa ni mbunge wa chama tawala ccm.

Proff jay alikuwa mbunge wa chama cha upinzani chadema.

Chama cha upinzani huwa hakiundi serikali hivyo hakitoi fursa kwa wabunge wake kuwa mawaziri
Ipo kwenye katiba au wanafanya kwa ajili ya maslahi yao tu mkuu
 
Sera wanazozisimamia haziendani, hivyo chama tawala hakiwezi kuwa na wabunge wa upinzani kwenye Serikali yao kwa nafasi ya uwaziri.
 
Vigezo vya Mteuzi unavijua?
Au kwa sababu wote ni Wasanii, unafikiri ndio kigezo cha kuwa Waziri/Naibu Waziri?
 
Jay hakuwa na watu kama Salaah nyuma yake
 
Hakuunga juhudi mkono kama angeunga hata angetaka kuwa spika enzi hizo angeinjoi
 
Hakuna serikali yenye macho kengeza. J alikuwa upinzani so Ccm(siwapendi) lakini hawawezi kumuweka mpinzani kwenye serikali yao hivyo hivyo chadema wangefanya kama wangekuwa madarakani
 
Kwani professor J alikuwa ccm?
 
Yule ni kada wa CHADEMA, unamlinganisha na mwana CCM Mwana FA?. Hata sugu angekuwa mwanachama wa CCM angeishapata uteuzi kule. CHADEMA haiko madarakani kutawala dola ndio maana mastaa walioko huko hawapati teuzi katika uongozi wa nchi
 
Mwanafa anastahili ukimuachilia Wakazi nadhani hao ndio wanaopambania haki za wasanii kuzidi wote.
 
Mbona swali jepesi?? Mawaziri wanatoka kwenye chama kinachoongoza dola
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…