Elections 2010 Mbona sioni watu wakisheherekea kuapishwa kwa rais wao mpendwa?

Kila wakifikiria hayo maumivu yanayokuja basi wanachanganyikiwa!:A S angry:
 
We Geni ukisema nyie mmesherehekea unamaanisha ni kina RIZ au nini??? hizo 61 za wapi? shake your brain well you will wake-up and start thinking If you wanna live longer otherwise hiyo kaputi itakuchukua moja kwa moja
 
Wafurahie nini wakati hawkuichagua, wamejichagua wenyewe so wanafurahia wenyewe mafisadi......kwa mtanzania wa kawaida ukiondoa mafisadi na watoto zao wanaona kuwa mkombozi wao Dr amedhulumiwa haki yake ya kuwaongoza na kuwaletea maendeleo
 

hawakumchagua, alipitishwa na wachakachuaji maarufu. Mimi kwangu TV haijawashwa tangu jana maana hakuna news.
 
Kila wakifikiria hayo maumivu yanayokuja basi wanachanganyikiwa!:A S angry:

Miaka mitano ya kulia na kusaga meno. Kwa mujibu wa JK Lengo la maisha bora kwa kila Mtanzania limeishatimia. kwa sasa anashughulikia KILIMO KWANZA kwa Ari zaidi, Nguvu zaidi na Kasi zaidi!!. Watanzania utadhani wameumbiwa maisha mabovu!! Hakuna kitakachobadilika katika maisha yetu kama hatubadiliki wenyewe na kuleta mabadiliko katika uongozi wa ngazi ya juu.
 
Furaha ni kitu cha Feelings, na feelings zaweza kua za furaha, uchungu, hatia na mengine. sasa kwa issue ya wana CCM mioyo inawasuta kwa madhambi waliyoyafanya.
Nakumbuka Mjini Arusha baada ya kutangazwa mgombea wa CHADEMA kua ni mshindi, mji wote ulirindimishwa kwa honi, na mbio za magari na pikipiki. na hata watumia daladala nao walionyesha mbwembwe za kila aina ikiwemo kupunga vidole viwili. kwa kweli ilikua ni sherehe ya aina yake. Sasa hii ya wenzetu wa CCM it is reflecting what is in their hearts. :A S angry::A S angry:na thambi hiyo itawatafuna kwa miaka yote hii mitano:A S angry::A S angry:
 

Ukweli gani utadhihirika. Unachemka. Huyo ni chaguo la watu mbona hata Chadema inasemekana wamechakachua, isitoshe Dr Slaa alikubali ameshindwa kwa kura 27000. kwani huji kushindwa ni kushindwa tu. Ngoja 2015 CCM nao watalinda kura zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…