Mzizi wa yote ni rushwa inayotolewa kwa wawakilishi wetu pale mjengoni,mishahara na marupurupu ya kutosha,halafu unamalizia miaka mitano na gratitude ya over 200 millions Tshs in cash instantly on last day of the fifth year.Ndiyo maana wapo tayari kwa lolote na kwa njia hata zile zisizo halali kuupata ubunge,watu wanaachia ofisi za umma zinazohitaji visomo vyao na kwenda kusema ndiyooo huku wakiishi kifalme,wanajipangia mishahara na posho nono na kusahau vipaumbele vya Watanzania.
Tunahitaji mabadiliko,tuseme inatosha kwa ukosefu wa umoja,mshikamano,usalama,uhuru wa maoni na kutofautiana kwa hoja bila kugombana.Sisi sote,bila kujali itikadi zetu ndiyo Watanzania,tunajenga nyumba moja,ya nini tugombee fito?Kila mmoja wetu ni potential,msijimilikishe ujenzi wa Taifa.Uongozi siyo Utawala bali Utumishi wa Wito.Hakuna aliye bora kuliko mwingine,usawa wa binadamu na haki za binadamu ni msingi wa UTU.