Mbona wachina wapo kila sehemu nchini! Serikali iwadhibiti

Mbona wachina wapo kila sehemu nchini! Serikali iwadhibiti

KweliKwanza

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2016
Posts
3,520
Reaction score
2,816
Kila sehem wapo, Magerage wapo, maduka, karikoo wanaanza kuishika, mitaani wamejaa, kwenye viwanja vya ndege wapo, Mabondo ndo wamewekana kila level, yani humuuzii mchina wa juu bila kuwauzia wachina wa mitaani. Vidispensary wamevijaza kila kona

Hawa wanaongezea dola kupanda maana wanachuma hela na kuziba mianya ya waTanzania mwisho wanabadilisha hela yetu wanaondoka na dola.

Hivi serikali yetu ni serikali inayopenda mema ya waTanzania au mema ya wachina

Naiomba serikali iingilie kati kiukweli
 
Hakuna udhibiti wa Wageni, uhamiaji Bize na kuwanyima watu pasopoti.wanaacha wachina wanazulula kama maembe sindano.
Wamejaa sana, badae ndo unashangaa wameshika kila kitu waafrica wanabaki vidampa, na wanadharau sana waafrica
 
Yaani hadi vijijini wamejaa wao tena wanaendeaha vitega uchumi muhimu
 
Wakichukua nyumba wanalala kibao hata 50 kwenye nyumba moja hawafai kupangishwa nyumba hao.
 
Nyie mmekatazwa kwenda China?

Unajua kuna wabongo wangapi China?

Mna mawazo ya kijima sana.

Screenshot 2025-01-21 055418.png
 
Tunakokwenda tutakuwa kama Africa Kusini.
Vijana wetu watakapoona ajira na fursa za kutengeneza maisha zinachukuliwa na wageni,huenda wataleta vurugu kuwavurumisha wageni kwa mawe.
 
Yaani kama tungekuwa hatupendi hela za rushwa hawa wasingekuwepo hapa
Yaani muwekezaji anauza maua?
Mhabeshi anakamatwa na kupigwa mapicha kama muuza madawa kumbe kakimbia kuuwawa kwao

Wachina wangedhibitiwa na visa wangesema tunawapa wataalamu tu
Ila kwa kuwa tunaweka matumbo mbele kuiuza nchi ni rahisi sana
Nilienda Cairo miaka ya nyuma sana
Nikampa dereva wa taxi $100 akaniambia chukua Cairo yote 😄
 
Kila sehem wapo, Magerage wapo, maduka, karikoo wanaanza kuishika, mitaani wamejaa, kwenye viwanja vya ndege wapo, Mabondo ndo wamewekana kila level, yani humuuzii mchina wa juu bila kuwauzia wachina wa mitaani. Vidispensary wamevijaza kila kona

Hawa wanaongezea dola kupanda maana wanachuma hela na kuziba mianya ya waTanzania mwisho wanabadilisha hela yetu wanaondoka na dola.

Hivi serikali yetu ni serikali inayopenda mema ya waTanzania au mema ya wachina

Naiomba serikali iingilie kati kiukweli
watz nunueni ardhi , very soon migogoro mikubwa itaanza
 
Niliona wachina 2 na wabongo3 wanauza sola kijijini mji kwa mji mguu kwa mguu.Hongera sana wachina wana akili sana wanajua hadi kusalimia kisukuma.
 
Niliona wachina 2 na wabongo3 wanauza sola kijijini mji kwa mji mguu kwa mguu.Hongera sana wachina wana akili sana wanajua hadi kusalimia kisukuma.
Niliwakuta mtaa mmoja hivi wana pickup imejaa Home appliances, wanauza kwa kupita nyumba kwa nyumba, unawapa kianzio then wataijia ilobaki, huku wabongo tunasubiri wateja waje dukani mchina anawafata nyumbani.
 
Hiyo iko wazi jamaa wanakunywa maji kandoro wala hawawazi kabisa na walisema watu kuwa wanalala hukohuko kwenye miji ya watu mkikubali kuwahifadhi.
 
Back
Top Bottom