Mbona wanariadha wa Tanzania wa mbio ndefu hawamalizi mbio hizo?

Huko ni olympic
Sasa na huko kwenye ndoa zenu hali ni mbaya
Uzuri tumekula kiapo tulinde taarifa zenu
 
Tutengeneze wanariadha wengi zaidi ili tujue ni yupi anaweza kumaliza mbio au kuacha njiani…
 
Tumebakiwa na wanariadha wawili wa kiume tegemeo wa mbio ndefu…wengine wanajikongoja tu
 
Nadhani ni misosi tunavyokula,tunaita vya asili but makande ni chakula kizito sana.Mzungu yy anakula biskuti na maziwa mbio zake tutaziwezea wapi?
 
Ni kweli kabisa. Hakuna maandalizi ya kutosha, na pia lishe Bora hawapati.
Unaongea tu siasa wewe. Mwanariadha milionea kama Geay mwenye ufadhili wa Adidas akose lishe? Punguzeni ujuaji kwenye mambo msiyoyajua.
 
Unaongea tu siasa wewe. Mwanariadha milionea kama Geay mwenye ufadhili wa Adidas akose lishe? Punguzeni ujuaji kwenye mambo msiyoyajua.
Hivi unajua maana ya kambi wewe?!
Kwenye kambi kuna wataalamu wa fani mbali mbali k.m. mazoezi, tiba, lishe n.k.

Unaweza kuwa milionea lakini usielewe lishe gani unayotakiwa kutumia.

Ukiangalia hata wachezaji wa timu za Ulaya na za kwetu huoni tofauti? Lishe zao zinasimamiwa na wataalam wa nutrition.
 
Wanaogopa wakimaliza hawatakwenda kushiriki tena.
 
Bado nakuona mpiga siasa kwa sababu hujui hata jinsi professional athletes wanavyoishi. Daraja alilopo kwa sasa huyo Geay hayo yote unayosema anayafanya na zaidi. Kabla hata ya serikali huwa Club yake inamwongoza kwenye kila kitu. Hizo kambi za mwezi mmoja zinazofadhiliwa na serikali huwa zina mchango mdogo sana kwenye kipaji chake. Ndo maana hata kwenye mpira inashauriwa nchi iwe na wachezaji wengi wanaocheza Ulaya ambako wanajua nini maana ya professional footballler. Kambi za Taifa Stars ni bure kama haina wachezaji wanaochezea Club za Ulaya.
 
Nimeshaona nabishana na mtu ambaye anabisha tu for the sake of it.

Kama athletes wa Kenya wanaweza kudominate kwenye International competitions kwa nini sisi tushindwe?

Unadhani ufumbuzi ni kumwacha Kila mchezaji ajisimamie mwenyewe?
 
Nimeshaona nabishana na mtu ambaye anabisha tu for the sake of it.

Kama athletes wa Kenya wanaweza kudominate kwenye International competitions kwa nini sisi tushindwe?

Unadhani ufumbuzi ni kumwacha Kila mchezaji ajisimamie mwenyewe?
Hilo swali la kwanza kwamba kwanini sisi tushindwe ni swali zuri na ninakupongeza. Kuna sababu nyingi sana ila sababu kubwa ni serikali kutotia juhudi za kutosha kwenye kuibua vipaji. Swali la pili ni la hovyo na halina maana yoyote ila tambua kwamba hata hao wakenya hawasimamiwi na serikali. Wana timu zao. Au unadhani mwanariadha anavyokimbia pale kajiendea tu peke yake? Nyuma yake ana management inayomsimamia.. na hata hela za zawadi na malipo mengine kuna wadau wana chao pia. Professional athlete ni kama mtoto. Husimamiwa kila kitu hadi chakula na muda wa kupumzika. Wana ratiba za kulala mchana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…