Mbona wasema kosa langu?

Mwanakijiji inawezekana kabisa hakuwa moyoni mwako wewe kwa sababu kama alikuwepo ni wewe ambaye ulitakiwa kuiondoa ile "kaka" aliyokuwa anakuita, ni wewe ambaye ulitakiwa kuuvunja ukimya umesahau mabinti wa enzi hizo hawakuwa na ujasiri wa kujitokeza na kung'ara kama kiwi!!

Sikitika tu kisha uende zako kwani si wako ni wa mwenzako.
 
Sasa akimletea mumewe vitimbi akaachika akitumaini tutakuwa pamoja itakuwaje? Oh well..haya mambo nasikia hayana kanuni..

Kwani wewe uko tayari kubeba mzoga(dead ball?)
Akiachika huyo hakufai tena, nadhani wewe unahitaki kitu kipya, na si mtu aliyeshindikana.
Go higher bana, huyu tayari yuko low kwako, anakutafutia risk.
 
Kwani wewe uko tayari kubeba mzoga(dead ball?)
Akiachika huyo hakufai tena, nadhani wewe unahitaki kitu kipya, na si mtu aliyeshindikana.
Go higher bana, huyu tayari yuko low kwako, anakutafutia risk.

Mh!!
 
hao wa namna hiyo
wallah ni wa kupotezea
kwani huja na hiyo
ili kujikombelea
mwanakijiji epuka, hizo ndumi la kuwili

kumbukumbu yasema
natakastaki uchovu
ungejaribu kusema
ungeshatolewa povu
huwa wajifanya wema, ili umwage upupu

nna hakika nasema
kazi yao kulalama
hasa wakikosea
pale wapoozea
mwanakijiji cheua, wala usimjali

siku zote twasema
ya kale hayana tija
na kama hii awali
basi awali mbovu
we mchomeshe mahindi, asirudie lawama
 
Kwani wewe uko tayari kubeba mzoga(dead ball?)
Akiachika huyo hakufai tena, nadhani wewe unahitaki kitu kipya, na si mtu aliyeshindikana.
Go higher bana, huyu tayari yuko low kwako, anakutafutia risk.

PJ uko righ kabisa, huyo anahamisha magoli... keshanyea kambi huko na moto wa kifuu sasa anatafuta matatizo.... labda MMM ashtue halafu apotezee kiaina
 
miye hata sijui; you know what.. let me sleep on it (naombea niote jinamizi)..
 
MM naona unajitafutia kujijustify! endelea but unajua la kufanya...!
 
Kwani mke wa mtu hamegeki? Kwa taarifa yako hao ndio huwaga watamu zaidi...

Mkulu,

Haya maisha yako very ironic.

Yaani ukimega mke wa mtu leo,basi nakupa 120% wako pia atamegwa au anamegwa au kama hujaoa ukio atamegwa tu.
Hata vitabu vya dini vinasema hivyo.
 
πŸ™‚πŸ™‚πŸ™„πŸ˜Ž
 
Sasa akimletea mumewe vitimbi akaachika akitumaini tutakuwa pamoja itakuwaje? Oh well..haya mambo nasikia hayana kanuni..

hata akija kwako utegemee vitimbi pia, hana msimamo! akishavunja ndoa yake coz ya mwanaume mwingine utegemee lolote kwa mwanamke wa dizaini hii.
 
Angalizo: Wako dada zetu wengi tuu wana maisha mzuri, nyumba, gari, pesa lakini wako kwenye mateso ya moyo, hivyo vingine vyote ni bure, ukimsaidia mtu wa aina hii hata kwa liwazo tuu la moyo 'not doing', unapata baraka kwa Mungu.

Hiyo si sawa na kumwonyesha chakula mwenye njaa? Anaweza kujitwalia chakula kwa nguvuπŸ™‚!
 
jamani labda wewe ulikuwa uko very serious binti alijaribu kuonyesha hisia lakini haukuona hizo hisia Ulifumbwa na neno kaka ..
lakini si ndo maadili yamejengeka eti nyie mtuanze na sio sisi tuwaanze cause tukiwaanza tutaonekana vicheche
pole dada it iz your time to move on with u life ,fogeti about Mwanakijiji yuko katika ulimwengu mwingine sasa,,

Mmenikumbusha ile Movie ya Julia na cameroon -My best friend wedding !!
 
Sasa akimletea mumewe vitimbi akaachika akitumaini tutakuwa pamoja itakuwaje? Oh well..haya mambo nasikia hayana kanuni..

Ukimuonja anaweza kujikuta anafanya hivyo. Ndio maana wadau wanasema usionje tafadhali! Kama uliweza kuvumilia enzi hizo akiwa bado mbichi, utashindwaje sasa?
 
Mkuu nimefurahi sana kuona mada nyeti kama hii ikitoka; sikutarajia. Kweli JF ni dawa. Mie pia nikiwa mmoja wa watu wa enzi "hizo" nimetokewa na masahibu ya aina hii. Ila kusema kweli, kwangu mie ni kwa mtu niliyekuwa nikitamani sana kumtolea ombi lakini akinionyesha kutokuwa na interest ya kwenda mbali na mimi zaidi ya urafiki wa kawaida. Ujasiri ukapotea. Nilikuja pigwa na butwaa baada ya miaka kadhaa, wote tukiwa tayari na familia zetu, kusikia akinilaumu kuwa sikumthamini miaka ile.

Wengi wametoa maoni yenye mantiki sana humu. Nadhani baada ya kuishi kipindi inatokea binadamu tuna hulka ya kutathmini maisha yetu na, with the benefit of hindsight, tunatamani kama tungefuata au kuchagua option nyingine tofauti na tulivyoamua tukifikiri mambo yangekuwa bora zaidi.

Nionavyo, mkuu hakuna cha kulalia changamoto hili labda tu, kama walivyogusia wataalamu humu, wataka kuvunja amri ya sita kitu ambacho kinaweza kukuletea taabu zaidi ikiwa ni pamoja na kuwaathiri nyote kisaikolojia. Dawa hapa ni kuendelea kuweka ukuta kama mwanzo na kuangalia mbele. Maji yalishamwagika. 😎
 
Kumbe na wewe umemuona eh?...... tena anasema anakwenda kulilalia ili aoteshwe lol

Mwanakijiji kaka yangu umenasa!

MJ1 mbona unazidi kumkwaza Mwanakijiji? Hilo la kuitwa kaka ndilo lilimponza akakosa tunda ''enzi hizo''.
 
Ukimuonja anaweza kujikuta anafanya hivyo. Ndio maana wadau wanasema usionje tafadhali! Kama uliweza kuvumilia enzi hizo akiwa bado mbichi, utashindwaje sasa?

Masaki uko likizo? maana siku hizi mahudhurio yako mazuri!!

Ushauri mzuri huu
 
Masaki uko likizo? maana siku hizi mahudhurio yako mazuri!!

Ushauri mzuri huu

Hapana, ni wiki hii tu mwajiri kalegeza kamba kidogo! Next week ukitaka kuniona online itabidi unitafute kule kwingine! πŸ™‚
 
MJ1 mbona unazidi kumkwaza Mwanakijiji? Hilo la kuitwa kaka ndilo lilimponza akakosa tunda ''enzi hizo''.

We nawe yaani hata kama ndo ku-read between lines wewe umezidi sijui una-read between words?

Eti kaka Masaki lol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…