Mbona watu hawajadili kuhusu kumiliki ndege, helikopta au meli na boti

Mbona watu hawajadili kuhusu kumiliki ndege, helikopta au meli na boti

Kumiliki ndege au helikopta sio jambo la kuamka asubuhi na pesa zako ukanunua helikopta au ndege zako ukaanza kuruka angani.

Kuna vigezo, masharti, kanuni na taratibu za kisheria lazima ukidhi na ufuate.
 
Habari za muda wakuu. Najua mko powa kabisa

Ningeomba kujua mbona watu hawajadili kuhusu meli au boti. Au mtu anayetamani kumiliki ndege au helikopta au ndo mimi sijawahi kuona nyuzi humu.Msaada tafadhari.....
 
Habari za muda wakuu. Najua mko powa kabisa

Ningeomba kujua mbona watu hawajadili kuhusu meli au boti. Au mtu anayetamani kumiliki ndege au helikopta au ndo mimi sijawahi kuona nyuzi humu.Msaada tafadhari.
Kwani we unataka boss?
 
Ukienda Dar au Mwanza kuna Yatch club utakuta boat za matajiri
 
Kama nini na nini tufahamu mkuu....?
Air operator certificate kutoka kwa mamlaka ya usafiri wa anga(TCAA).

Radio license certificate.

Qualified personnel. Crews. Na uwe na kipato cha kutosha kuwalipa.

Pia kuna gharama zingine utatakiwa kuzilipia kama Navigation fees, Mafuta ya ndege, parking fees n.k
 
Air operator certificate kutoka kwa mamlaka ya usafiri wa anga(TCAA).

Radio license certificate.

Qualifed personnel. Crews. Na uwe na kipato cha kutosha kuwalipa.

Pia kuna gharama zingine utatakiwa kuzilipia kama Navigation fees, Mafuta ya ndege, parking fees n.k
Kwa mfano wa helkopta ambayo inaweza kupaki hata katika eneo langu nayo hutozwa hiyo parking fee bila kujalisha imepaki Kwa mmiliki au laa ! Najibu tafadhali mkuu
 
Mkuu ikiwa hizi ndoto tulizo nazo za kumiliki magari, bado ni mgari ya 2006 huko, je unadhani kumiliki ndege itawezekana kirahisi? Hadi tuwe na hizo ndoto.
 
Kwa mfano wa helkopta ambayo inaweza kupaki hata katika eneo langu nayo hutozwa hiyo parking fee bila kujalisha imepaki Kwa mmiliki au laa ! Najibu tafadhali mkuu
Kama utaweza kuandaa eneo lako la kupaki helikopta yako huwa wanaita (Helipad) inaruhusiwa kufanya hivyo.

Lakini utakapokuwa unaingia maeneo ya Airports itahitajika uwe unalipia parking fee.
 
Back
Top Bottom