Mbongo akikuambia Lori ya Tandamu basi elewa kama ifuatavyo...

Mbongo akikuambia Lori ya Tandamu basi elewa kama ifuatavyo...

Asante,
Binafsi nimelisikia sana, na mawazo yangu ilikua ni gari yoyote kubwa inayobeba mizigo,
Kuna watu hata fuso huita Tandam.
Hilo neno kinatumika sana kwenye fuso kutofautisha tani 10 na 15
 
Utakuwa wa ushuani wewe sio bure mkuu...hili ni neno maarufu sana kwenye sekta ya usafirishaji tanzania hasa kwenye magereji, masoko makubwa ya mazao kv mahindi nk

Kuna terminologies fulani kama hauko vizuri sana kwenye ku-socialise huwezi zifahamu kabisa!!
Mimi mwenyewe pia silijui mkuu na wala sio wakishua
 
Dah...umenikumbusha...kuna siku nilikaa na madereva wa mabasi ya mkoa...sikuambulia kitu kwenye maongezi yao...kwani maneno kama chips kavu..maini rost..slesi tupu ndiyo aina za mabasi [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hahah
 
Jamaa wana misamiati yao utasikia "mnara" "mahakama" basi we utajua mahakama kweli!!
Mnara najua maana yake ... Mara ya kwanza kusikia hilo neno nilikuwa siwaelewi kabisa
 
kweli kiswahili ni kipana

yani hili neno ni maarufu ila ndio kwanza nalisikia leo
 
Nakumbuka chuo pisi zilizojaa tulikua tunaziita "RUTANDAM" nilikua sijui kwanini cause mimi mwenyewe nililikuta tu hilo neno now i know why!
 
Back
Top Bottom