Mbosso badilika, gemu itakushinda

gonamwitu

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
2,187
Reaction score
2,794
Ahlan wasahlan wanajukwaa,

Huyu kijana wa kuitwa Mbosso "Khan Mushedede" kutoka viunga vya WCB kiundashi, melody na hata jinsi anavyoimba yuko njema.

Shida yake ni moja tu: habadiliki, kila siku nyimbo zile zile, uandishi ule ule, mahadhi yale yale. Kila wimbo anataja maandazi, kachori, chapati, mishikaki; mara nisugue, mara nikande, mara nibebe, mara niteme n.k.

Kiukweli inabidi abadilike kama anataka kufika mbali na kudumu kwenye gemu kwa muda mrefu. In short, mashabiki wamemchoka. Ushahidi ni huu wimbo wake mpya wa ate; mahadhi yale yale, uandishi ule ule, hadi mashabiki wameamua kumchana abadilike wamemchoka.

Yangu ni hayo tu.

"Njoo kichwa kichwa ule za uso saba"
 
Kweli aisee..... Kama mm si mshabiki sana wa aina ya muziki anaoimba..,yaani uko kitaarab hivi.... Anatakiwa abadili ladha... Mbona bro domo anatupa ladha tofauti tofauti....hawamwigi hata bosi wao...
 
Jamaa ana uwezo mkubwa Sana na uwezo wa kubadilika anao mfano ngoma Kama shida, alele na picha yake ameonesha utofauti sana nilitegemea ataendelea hivyo hivyo badala yake karudi Tena kwenye uhindi ebu ajifunze kwa rayvanny.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…