Mbosso(WCB) vs Aslay, nini kitatokea?

GadoTz

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2014
Posts
370
Reaction score
636

Kwa wasiomfahamu Marombosso ni kijana hapo kwenye video, ambae alikuwa miongoni mwa wanaounda Yamoto band.

Kwa sasa ametoka kupitia WCB.

Wakati yupo Yamoto walikuwa wanachuana vikali na Aslay na inasemekana ni moja ya sababu kundi kuvunjika ni hivi vipaji viwili.

Kwa kutazama muono wa mbali tutarajie mchuano mkali ambao siwezi kuuita bifu bali ni mchuano wa vipaji toka kwa aslay na mbosso.

Nini kitatokea baada ya mchuano huo kuanza rasmi? Tuvute subira.
 
Mboso ni hatari sanaaaa,yamoto band ilikia inajengwa na aslay na mboso,ndo mana watu walishangaa kwa nn mboso hatoi nyimbo muda mrefu,so si wa kumpuuza huyu bwana Mdogo ana sauti amazing sana,Nikikimbuka vipengele vyake anavyochanaga daaaah
 
Aslay amesimama mwenyewe bila lebo kubwa, leo hii ameshakuwa msanii mkubwa nyimbo nyingi show ya mtu mmoja inaenda, leo hii unamfananisha na mbosso kweli mkuu? Mpe heshima yake
Hakika Mkuu!! Watani wangu wangeuliza "Mboos Whoooo??! Mboos Whaaat?"
 
Waganga wa kienyeji watanufaika zaidi
 
Mleta mada angalau umeleta mfananisho unaoendana!!

Sie wengine tulikuwa tunaangalia tu walivyokuwa wanajaribu kumpambanisha Aslya na Diamond baada ya kuwa wameshindwa kwa Darasa!!! Tukaonya hapa, msimvimbishe kichwa dogo akajiona tayari ameshakuwa heavy weight manake yupo bado sana kuweza kumshindanisha na mtu mwenye fans base ya kufa mtu Afrika Mashariki yote and beyond!

Watu wakamjaza... wakamjaza... nasikia hivi sasa analia lia! Mara aandike barua kwa mama... mwanamuziki unaandika barua kwa mama badala ya kutunga wimbo kwa mama kumwelezea maswahibu yako!!!

Waliojulia muziki ukubwani wanadhani muziki is all about kuingia studio na kutoa hit song! Yes, muziki upo hivyo... lakini hakuna muziki pasipo tasnia ya muziki!

Na kwa kujibu swali la mleta mada, Maromboso atampoteza Aslay kwa sababu Mboso amezungukwa na watu wanaojua muziki na tasnia ya muziki!

All in all, I cry for Beka Flavor...
 
Ama kwa hakika wengi awaujui moto wa mbosso khan aka mshedede. dogo anaimba utafikiri bob marley kazaliwa upya. akiimba live usipotoka vipele wewe mwanaume
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…